Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

TARURA KUONGEZA MTANDAO WA BARABARA ZA LAMI KM 1,450, CHANGARAWE KM 73,242’ ENG. SEFF

Imewekwa tar.: August 14th, 2022

OR-TAMISEMI

Mtendaji Mkuu wa TARURA Eng. Victor Seff amesema kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2026/27 lengo ni kuongeza mtandao wa barabara za lami kwa km 1,450.75  kutoka km 2,404.90 zilizopo hivi hadi kufukia Km 3,855.65, changarawe km 73,241.57  kutoka km 29,116.57  hadi kufikia km 102,358.14 na madaraja 3,808  kutoka  2,812 hadi  kufikia madaraja 6,620.

Aidha, amebainisha kuwa fedha zitakazotumika kwenye mpango huu zinakadiriwa kuwa zaidi ya Shilingi trilioni 4.2.

Eng. Seff ameyasema hayo kwenye hafla ya Utiaji Saini Mikataba baina ya Wakandarasi wa Ujenzi wa Miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na TARURA kwa mwaka wa Fedha 2022/23 uliofanyika kwenye  ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center mapema leo Tarehe 14.08.2022 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

‘Mpango Mkakati wetu wa pili ni kuwa ifikapo 2026/27 asilimia 85 ya mtandao wa barabara za Wilaya chini ya TARURA zitakuwa zinapitika kwa misimu yote na nyakati za mvua hapatakuwa na taharuki inayojitokeza sasa kwa maeneo mengi kujifunga.

Hii pia ina akisi kauli mbiu yetu ya Mpango Mkakati wa pili inayosema

TARURA TUNAKUFUNGULIA BARABARA KUFIKA KUSIKOFIKIKA’ alisisitiza Eng. Seff

Aliongeza kuwa Katika utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2022/23 jumla ya zabuni 1,706 zitatangazwa zenye thamani ya Shilingi 621.66 zilipangwa kutangazwa. Kwa awamu ya kwanza tulitangaza asilimia 60 ya bajeti sawa na zabuni 1,085 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 378.56, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo toka Ofisi yako TAMISEMI ya kufanya ununuzi wa asilimia 60 ya bajeti ili kazi zianze mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza na pia tumeanza utekelezaji wa awamu ya asilimia 40 iliyobaki.

Kati ya zabuni 1,085 zilizotangazwa katika awamu ya kwanza, leo utashuhudia uwekaji wa saini mikataba 968 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 331.39. Zabuni nyingine zipatazo 117 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 47.17 zimerudiwa kutangazwa kutokana na kukosekana kwa Makandarasi wenye sifa maeneo hayo.

Jukumu kubwa la TARURA ni kusimamia Ujenzi/Ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za Wilaya wenye jumla ya kilomita 144,429.77. Kati ya urefu huo, kilomita 2,635.75 (1.82%) ni barabara za lami, kilomita 32,504.26 (22.5%) ni barabara za Changarawe na kilomita 109,289.77 (75.67%) ni barabara za udongo.

Pia kuna jumla ya Madaraja 3,191 na Makalavati 69,317 Hali ya mtandao wa barabara za Wilaya hadi kufikia Juni 2022; asilimia 23.6 (km 34,056) una hali nzuri, asilimia 33.7 (km 48,684.36) una hali ya wastani na asilimia 42.7 (km 61,689.42) una hali mbaya.

Kama takwimu zinavyoonesha, asilimia 75.67 ya mtandao wa barabara za Wilaya ni za udongo na zinaathirika sana wakati wa misimu ya mvua na kusababisha maeneo mengi kutopitika.



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.