Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

SILINDE: KITONGOJI CHA NKANKA KUPATA SHULE, BARABARA

Imewekwa tar.: October 26th, 2022

OR -TAMISEMI ILEJE

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amesema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuridhia wananchi wapatao 3,000 wanaoishi katika hifadhi ya msitu wa Ileje Renger katika kitongoji cha Nkanka Kijiji cha Itumba wilayani Ileje kuendelea kubaki Serikali itaanza ujenzi wa shule  shikizi ya msingi na barabara.

Mhe. David Silinde ameyasema hayo  leo  Oktoba 25, 2022  katika  ziara ya  kamati ya mawaziri wa kisekta inayoshughulikia migogoro ya Ardhi ilipokuwa inaongea wananchi wa kitongoji cha Nkanka, ambao kitongoji hicho kipo katikati ya hifadhi ya msitu wa Ileje Renger na ambao wameishi hapo kwa zaidi ya miaka 40.

Mhe. Silinde amesema baada ya mchakato wote kukamikika, ujenzi wa shule ya msingi shikizi utaanza na badae itasajiliwa kuwa shule kamili kwa kuwa ni dhamira ya mheshimiwa Rais  kumaliza changamoto zote za miundombinu kwenye sekta ya elimu.

Mhe. Silinde amesema ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo 2027 changamoto za miundombinu kwenye elimu nchini ziwe zimemalizika kabisa na analeta fedha nyingi za kumaliza changamoto za miundombinu kwenye elimu.

Mhe. David Silinde amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI inasimamie miradi nmikubwa ya kutatua changamoto za miundombinu katika elimu hapa nchini, ukiwemo mradi Boost una fedha zaidi ya tirioni 1.1 ambazo kazi yake ni nikuboresha elimu ya msingi kwa kujenga shule mpya na kuboresha zilizopo, mradi wa SEQUIP kwa ajili ya kujenga Sekondari mpya kwenye kata ambazo hazina,  mradi wa lipa kulingana  na matokeo (EP4R)

Kuhusu Barabara ya Nkanka, Mhe. Silinde amesema baada kumaliza changamoto TARURA Ileje watakuja kuisajili ili Serikali itoe fedha na iweze kutengenezwa vizuri.

Agnes Nyondo mwananchi wa kitongoji cha Nkanka amesema baadhi ya viongozi kuwaambia wahame wamejikuta wanashindwa kufanya mambo ya maendeleo, kama kujenga ,na kulima kwani wamekuwa wakiishi kwa hofu, hivyo wamemshukuru  Rais Samia kwa uhamuzi wake wa kuwataka wabaki katika eneo hilo

Ephraim Kayinga mkazi wa kitongoji cha Nkanka amewaomba mawaziri kuwafikishia salama kwa Rais Samia kwa uamuzi wake wa kuwabakiza kwani wao wamezaliwa Nkanka na maisha yao yoote yamekuwa hapa.


MWISHO


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NENDENI MKAITANGAZE SERIKALI.

    May 24, 2025
  • SOKO LA KISASA LA NYAMA CHOMA LAZINDULIWA VINGUNGUTI

    May 24, 2025
  • DKT. Biteko asisitiza wazazi kuthamini nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya mtoto.

    May 24, 2025
  • Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha  huduma ya afya ya msingi.

    May 24, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.