Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Shule za vijijini zaula ajira mpya 13,000 za waalimu.

Imewekwa tar.: November 27th, 2020

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema Serikali imewapanga zaidi waalimu wa shule ya msingi katika shule za vijijini ambako ndiko kwenye upungufu mkubwa zaidi ya waalimu.

Akiongea na vyombo vya habari leo kuhusu ajira mpya za waalimu wa shule za msingi na Sekondari pamoja na mafundi sanifu wa maabara Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa kwa upande wa shule za msingi  upangaji wa waalimu umefanyika kwa lengo  la kuboresha  uwiano wa waalimu kwa wanafunzi.

Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa asilimia 60 ya walimu wote walioajiriwa wamepelekwa katika shule za msingi hasa za vijijini ambako ndipo kwenye uhitaji mkubwa wa waalimu nchini.

Ameendelea kufafanua kuwa Serikali imeweka kipaombele kuajiri waalimu kwa ajili ya shule za sekondari zenye mchepuo wa sayansi na Hisabati, ufundi, kilimo na maarifa, maarifa ya nyumbani, lugha ya kingereza, kichina na kifaransa.

Amesema kuwa walimu wa masomo mengine wamepangwa kulingana na upungufu uliopo ambapo kipaombele ni shule ambazo hazina walimu wa masomo husika.

Mhandisi Nyamhanga amesema pia wamezingati shule zenye mahitaji maalum ambako waalimu 481 wameajiriwa kwa ajili ya shule hizo na kuwa suala la umri wa ajira za Serikali limezingatiwa kwa waalimu waliopata ajira ni wale waliomaliza chuo mwaka 2014 mpaka 2019.

Aidha Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa waajiriwa wapya  wa uwaalimu  wa shule za msingi na Sekondari wanatakiwa kuhakikisha wanaripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya muda wa siku 14, kinyume na hapo watakuwa wamepoteza  nafasi zao na zitajazwa na waombaji wengine.

“waajiriwa wapya  wanatakiwa  kuripoti kazini  kuanzia tarehe 1 hadi  tarehe 14 Desemba 2020  watakaoshindwa kuripoti nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa waliopo kwenye kanzidata ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI”, amesisitiza Mhandisi Nyamhanga.

Vile vile amewaagiza  wakurugenzi wa Halmashauri ambao walimu hao wamepangiwa kuwapokea na kuwawezesha  kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma.

Hata hivyo amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatoa taarfa ya kuripoti waajiriwa hao na kuzijaza kwenye mfumo wa Elektroniki baada ya kila mtumishi kuwa amepokelewa katika kituo cha kazi.

“Kamilisheni mtaratibu za ajira haraka ili walimu hawa waingizwe katika mfumo wa malipo ya mshahara(payroll) mapema iwezekanavyo”, ameelekeza Mhandisi Nyamhanga.

Tarehe 7 Septemba, mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alitoa kibali cha ajira mpya za walimu 13,000 wa shule za Msingi na Sekondari pamoja na Mafundi Sanifu wa Maabara za Shule.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.