• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Shilingi milioni 700 kujenga Madarasa 100 Mwanza, Morogoro na Dodoma

Imewekwa tar.: July 19th, 2019

Na Mathew Kwembe, Mwanza

Serikali imelipongeza shirika lisilo la kiserikali la children in Crossfire kwa mkakati wake wa kujenga madarasa ya elimu ya awali 100 katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara katika kijiji cha Magaka, wilayani Misungwi wakati akizindua mojawapo kati ya madarasa manne ya elimu ya  awali kati ya madarasa 30 yanayojengwa katika wilaya za Misungwi na Ukerewe mkoani Mwanza.

Mhe.Waitara amesema kuwa kujengwa kwa madarasa hayo ya awali kutachochea ari ya watoto wanaojiunga na elimu ya awali kupenda kusoma na hivyo kupunguza utoro katika maeneo yanakojengwa madarasa hayo.

Mhe.Waitara ameongeza kuwa kama madarasa yenyewe yanayojengwa ni kama hayo aliyozindua anatumaini kuwa mikoa ya Mwanza, Morogoro, na Dodoma itakuja kuongoza kitaaluma katika miaka ijayo.

“Kama madarasa yenyewe ni yale tunaamini mikoa ya Mwanza katika wilaya za Misungwi na Ukerewe, pamoja na mikoa ya Dodoma na Morogoro inapaswa kuja kuongoza kwa taaluma ambayo wanaipata, na tunaamini kuwa watoto wataokuja kusoma katika madarasa haya watakuwa na uwezo mkubwa wa kimasomo,” amesema.

Amesema madarasa hayo ni ya mfano kwani siyo tu yanaongea, bali pia yanacheka na kutabasamu kwani kona zote za madarasa hayo zimesheheni zana mbalimbali za kujifunzia zinazomuwezesha mtoto siyo tu ajifunze kwa urahisi bali pia apende shule kutokana na kuwa na rangi za kuvutia.

“Hili darasa kama mlivyoona, nimekutana na madarasa yanayoongea lakini hili darasa linaongea, kutikisika na kucheka, na tabasamu linaongezeka,” amesema na kuongeza:

“Sasa nilikuwa napiga picha ya madarasa yanayoongea ambayo niliwahi kuonyeshwa pamoja na haya hapa, hongereni sana haya yametia fora.”

Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa sera ya mafunzo ya elimu ya mwaka 2014, Naibu Waziri amesema kuwa  kumekuwa na ongezeko la watoto wanaojiunga na elimu ya awali kutoka milioni moja mwaka 2015 hadi watoto milioni moja na nusu mwaka 2016.

Aidha Mhe.Waitara ameziagiza halmashauri kuhakikisha kuwa kila zinapojenga shule za msingi pia zinapaswa kuweka bajeti kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya awali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa shirika la kimataifa la Children in Crossfire bwana Craig Ferla amesema kuwa shirika hilo katika kipindi cha miaka mitano ijayo limepanga kutumia shilingi milioni mia 700 kwa ajili ya kujenga madarasa 100 ya aina hiyo katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dodoma.

Naye Mratibu wa mafunzo ya elimu ya awali kutoka shirika hilo bwana Davis Gisuka amesema kuwa mbali na kujenga madarasa hayo pia shirika lake  linawezesha kufanyika kwa mafunzo maalum kwa walimu wa shule za awali za serikali ili waweze kumudu kuwapatia elimu watoto wanaowafundisha kupitia mbinu mbalimbali za mafunzo ikiwemo matumizi ya zana rahisi za kufundishia zinazotengenezwa na walimu hao katika shule zao.

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.