• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Shilingi milioni 242 zatumika kukopesha vikundi 46 Tabora

Imewekwa tar.: March 9th, 2021

Na Paul Kasembo, Tabora

Manispaa ya Tabora imetoa shilingi milioni 242 kwa ajili ya kuvikopesha vikundi 46 vya wanawake, vijana na walemavu katika mwaka wa fedha 2019/20.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bosco Oddo Ndunguru amesema kati ya vikundi 46, vikundi 32 vya wanawake vilipokea mkopo wa shilingi milioni 160, vikundi tisa vya vijana vilipokea shilingi milioni 57 na vikundi vitano vya walemavu vilipokea shilingi milioni 25.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa Manispaa ameongeza kuwa Manispaa ya Tabora katika bajeti yake ya mwaka 2019/2020 ilitenga kiasi cha shilingi milioni 421 lakini zilizotolewa ni shilingi milioni 242.

Manispaa ya Tabora imekuwa ikitekeleza takwa la kisheria la kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.

Miongoni mwa vikundi vilivyonufaika na mkopo huo ni kikundi cha Upendo kinachoundwa na wanawake 11 ambacho kilianzishwa mwaka 2019 katika kitongoji cha Msangi Kijiji Cha Blockfarm katika Kata ya Kalunde.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kikundi hicho Aisha Salum, mwaka 2020 walipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka Mapato ya ndani ya Halmashauri uliowawezesha kujenga banda, kununua vifaranga 200, mbuzi pamoja na chakula cha kuku.

Mradi huo wa ufugaji kuku umewasaidia kuachana kabisa na kazi zisizo na staha ambazo awali walikuwa wakizifanya kwenye mashamba ya tumbaku.

Kikundi kingine ni cha wanawake Wagonga kokoto wa Kazehil Kata ya Ng’ambo mjini Tabora, kikundi kinachoundwa na wanawake 10 ambacho kilipata mkopo wa sh. Milioni tano kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri na sasa kinaendesha mradi wa kutengeza sabuni za mche (gwanji).

Mwenyekiti wa kikundi hicho Upendo Simon Meja anasema, “Lita 20 ya mafuta ya Mawese yanayotokana na zao la chikichi ikichanganywa na lita kumi ya mchanganyiko wa maji safi pamoja na acoustic soda wanapata miche ya sabuni kati ya 70 na 90.”

Vijana 10 wa kikundi cha Segehema kilichopo kata ya Ipuli mjini Tabora ambao wanafanya kazi za Useremala wamenufaika na mkopo wa shilingi milioni tano uliowawezesha kupata malighafi ya mbao na hivyo kuchonga samani za aina mbalimbali na kuziuza au kuzipeleka kwenye maonesho tofauti ikiwa ni sehemu ya kujitangaza na kutangaza bidhaa zao.

Vijana wengine wanaojishughulisha na kilimo katika Kijiji cha Kalumwa kilichopo Kata ya Uyui wamenufaika na mkopo wa shilingi milioni tano kupitia kikundi cha Umoja na hivyo kupanua kilimo cha nyanya na mpunga ambapo kwa sasa wamelima eneo lenye ukubwa wa jumla ya ekari 10 za nyanya na ekari 10 ya mpunga kwa maana ya kila mwanachama amelima ekari moja, moja ya nyanya na mpunga.

Aidha kikundi cha watu 10 wenye Ulemavu waliopo Kata ya Chemchem kupitia kikundi cha Chapakazi wamepata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka halmashauri ambapo kwa sasa wanajishughulisha na biashara ya usafirishaji.

Kikundi cha Twaweza kinachoundwa na wenye ulemavu nacho kimenufaika na mkopo wa halmashauri wa shilingi milioni tano na kuboresha shughuli zao za kuendesha Mgahawa wa Chakula katika eneo la Bombamzinga Kata ya Kiloleni.

 

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.