Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Shilingi Bilioni 3 zakwamua Wanawake, Vijana na Walemavu Geita

Imewekwa tar.: February 25th, 2021

Na Trovina Kikoti, Geita

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Halmashauri ya Mji wa Geita imetoa mikopo isiyo na riba ya shilingi bilioni tatu kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kila halmashauri nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhe. Costantine Morandi Mtani ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016 hadi 2020/2021 Halmashauri yake imefanya vizuri katika utekelezaji wa maagizo ya Serikali kutoa asilimia 10 ya bajeti kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Mhe. Morandi ameahidi kuwa Halmashauri yake katika awamu iliyoanza itaendeleza kasi ya utoaji wa mikopo hiyo kwa vikundi vyote vyenye mahitaji na nia ya dhati ya kutaka kujikwamua kiuchumi pasipo ubaguzi wa aina yoyote.

Kikundi cha Ufunuo kinachojumuisha vijana watano wa kiume wenye ulemavu wa aina mbalimbali walipata mkopo wa shilingi milioni 5 kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita ambazo walizitumia kuanzisha duka la rejareja na kufanikiwa kurejesha mkopo wote. Mwezi Julai 2019 walipewa mkopo mwingine wa shilingi milioni 20 ambazo walinunua gari dogo la kubeba mizigo maarufu kama kirikuu kwa ajili ya biashara ya usafirishaji mizigo.

Enos Lukubanija Kidubu, Mwenyekiti wa kikundi cha ufunuo ameishukuru Halmashauri ya Mji wa Geita na Serikali kwa ujumla kwa kuwawezesha kuendesha biashara ya usafirishaji ambayo inawapa faida kubwa na wamelenga kufikia mwaka 2025 wasiwe wategemezi tena, watajiimarisha kwa kununua magari mawili zaidi na kununua bidhaa muhimu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kama vile mafuta maalum ya ngozi na kofia za kutembelea juani.

Kikundi cha Wanawake cha Hongera ni moja ya vikundi vya wanawake chenye mradi wa kufuga kuku wa nyama na mayai pamoja na kuku wa kienyeji kinachofanya shughuli zake katika mtaa wa mission kata ya Kalangalala. Kikundi hicho kina wanachama watano ambao mwaka 2014 walipewa shilingi milioni 4 na Halmashauri ya Mji wa Geita na kufungua duka la vifaa vya redio na Televisheni, biashara yao ilienda vyema na kufanikiwa kuurudisha mkopo wote ukiwa na riba yake.

Mwaka 2019/2020 walipewa mkopo mwingine wa shilingi milioni 5 usio na riba ambao wmeutumia kuanzisha biashara ya ufugaji kuku wa nyama na mayai ambapo mpaka sasa wana kuku 500 zinazowapatia trei sita za mayai kwa siku. Mwezi machi 2021 watapokea vifaranga 400 vya kuku ili kukuza biashara yao.

Bi.Annastella Rweyemamu ambaye ni Mhazini wa kikundi hicho ameeleza kuwa faida wanayoipata kutoka kwenye biashara zao wanazitumia katika kutimiza majukumu ya familia zao, yeye binafsi amefanikiwa kujenga nyumba ndogo anayoishi na kuwasomesha watoto wake wawili walioko shule za Sekondari.

Mwaka 2019/2020 Halmashauri ya Mji wa Geita iliweka historia ya kutoa mkopo mkubwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa utaratibu wa utoaji mikopo kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa kutoa mkopo wenye thamani ya Shilingi Milioni 163 kwa kikundi cha Geita Youth kinachofanya shughuli zake katika mtaa wa upendo kata ya Bombambili. Mkopo huo ulitumika kwa ajili ya kununua roli aina ya FAW, Mashine mbili za kufyatulia matofali na fedha kiasi za kuanzia shughuli ya ufyatuaji wa matofali ya block.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Gabriel Nyasilu ameishukuru Halmashauri ya Mji Geita kwa kuwapatia mtaji huo kama walivyoomba katika andiko mradi wao ambapo hadi sasa biashara yao inaendelea vyema kwa sababu wamepata fursa ya kuuza matofali yao katika ujenzi wa miradi mbalimbali inayojengwa na Serikali, Taasisi na watu binafsi. Pia fedha wanazozipata katika biashara hiyo zinawawezesha kutimiza mahitaji binafsi.

Mratibu wa vikundi vya wanawake katika Halmashauri ya Mji Geita Bi. Valeria Makonda ameeleza kuwa changamoto kubwa anayokabiliana nayo kutoka kwa watu anaowasimamia ni mapokeo hasi kutoka kwa baadhi ya wanavikundi kuamini kwamba fedha inayotolewa na Halmashauri kama mkopo ni fedha ya hisani kutoka Serikalini ambayo haina ulazima wa kuirejesha licha ya elimu wanayowapatia kabla ya kupatiwa mikopo hiyo.

Bi. Makonda ameishauri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoa mpangilio(format) ya kudumu ya utoaji taarifa sahihi za ukopeshaji wa vikundi na kuandaa mafunzo ya mara kwa mara yatakayowasaidia wanufaika kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya kimkakati kama usindikaji wa vinywaji vitokanavyo na matunda. Pia mafunzo kwa wasimamizi katika ngazi ya halmashauri yatawajengea uwezo wa kuboresha usimamizi wa vikundi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.