Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

SERIKALI YATOA MIL. 250 ZA DHARURA KUJENGA DARAJA LA MBUGA, ULANGA

Imewekwa tar.: May 23rd, 2024



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amemuagiza Katibu Mkuu kuipatia TARURA kiasi cha shilingi milioni 250 za dharura kwaajili ya  kujenga daraja la muda la Mbuga katika mto Luhombero pamoja na ukarabati wa daraja la waenda kwa miguu la Chigandugandu wilayani Ulanga yaliyoharibiwa  kutokana na mafuriko.


Akizungumza na wananchi wa kata ya Mwaya na Mbuga ambao hivi sasa hawana mawasiliano na inawalazimu kutumia mtumbwi wa kuvutwa kwa kamba,Waziri Mchengerwa amesema kwa adha wanayopata wananchi hao daraja la muda haliepukili mahali hapo.


“Ndugu zangu kwanza tupate daraja la muda litakalowawezesha wananchi kupita wao wenyewe pia kupitisha mazao yao katika msimu huu wa mavuno,hatuwezi kutimiza malengo yetu kama daraja hili bovu”.


Waziri Mchengerwa amesema Kwa siku tatu za ziara yake kwenye wilaya zilizopata mafuriko mkoani Morogoro ameshuhudia  maeneo mengi yaliyopata uharibifu mkubwa wa miundombinu na kumuagiza  Katibu Mkuu kuipatia TARURA  milioni 250.


Hata hivyo alitoa maelekezo kwa  TARURA kuanza mara moja mchakato wa dharura wa ujenzi wa daraja hilo na kuwapa mwezi mmoja na nusu kulikamilisha.


Aidha, Waziri Mchengerwa aliwasıhi wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo kwani Rais anaendelea kuwajali wananchi wake na kuiangalia Ulanga hususani kwenye miundombinu.


“Fedha tunazoleta hapa ni fedha za  wananchi ambazo tunaelekezwa na Mhe. Rais,msingi wa serikali ni wananchi”.


Aliongeza kusema kwamba Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani itaendelea kuwajali wanyonge pamoja na wananchi wa Mbuga na Mwaya hivyo fedha za dharura zinazotemgwa zinaenda kutibu na  kuimarisha uchumi wa wananchi.


“Rais anawajali wanyonge na wananchi wake ndio maana akatoa fedha hizi kwa ajili kwa wananchi wake hususan maeneo ya uzalishaji na kimkakati ili wananchi waendelee kupata huduma pia wakulima wa mazao ya chakula na biashara waweze kuendelea na shughuli zao”.


Naye, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima ameaema daraja hilo ni la kiuchumi pia maisha ya watu wanahitaji daraja hilo kwani wakulima walikuwa wanatumia mtumbwi kuvusha mazao yao.


Amesema ni vyema kuanza kujenga vivuko vya muda katika mkoa wake ili kuweza kuwavusha wananchi na mali zao wakati wanasubiri kujengewa daraja la kudumu.


Awali Mbunge wa Ulanga Mhe. Salim Hasham amesema kata ya Mbuga ina watu wengi na ndio inayoongoza kwa uzalishaji wa zao la pamba na ufuta ambapo inaifanya Mahenge kuwa na zao la biashara.


Amesema licha ya matatizo ya Ulanga ni makubwa ila tatizo la daraja hilo ni kubwa zaidi  na amemshukuru Waziri kufika eneo hilo ambalo wananchi wa kata ya Mwaya na Mbuga walikuwa wakipata adha ya usafiri hususani wagonjwa.


Wakati huo huo Diwani wa Kata ya Mbuga Mhe. Said Mfaume amesema daraja hilo litakuwa mwarobaini wa kuwasaidia wananchi wa kata yake kwani kata hiyo inazalisha kwa 75% ya mazao ya biashara na chakula pia wakazi hao hupata huduma za afya upande wa pili wa Kata ya Mwaya.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

    June 14, 2025
  • MANYARA NA MWANZA MABINGWA RIADHA MITA 800 

    June 14, 2025
  • HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU  KATIKA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO- ADOLF NDUNGURU 

    June 13, 2025
  • WAVU KWAENDELEA KUNOGA UMITASHUMTA

    June 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.