Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali Yatoa Agizo Kukamilisha Ujenzi wa Kituo cha Afya Kibaoni

Imewekwa tar.: July 22nd, 2022

Na Fred Kibano, Mpimbwe Katavi

Serikali imeagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa kituo cha Afya kibaoni kilichopo Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe ifikapo mwezi Septamba ili wananchi wa eneo hilo wapate huduma za afya karibu na makazi yao.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kikazi wilayani humo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho hivi leo na kujionea hatua ya ujenzi iliyofikiwa na ndipo aliwataka watendaji kuongeza kasi ya ujenzi wa kituo hicho.

“dhamira ni ile ile, Mama Samia anachotaka ni kusogeza huduma karibu na wananchi, lakini nasisitiza tena madaktari, wahududumu wote wa afya mkawahudumie wananchi hawa kwa upendo, tumekubaliana na Naibu Waziri TAMISEMI mwezi wa tisa kukamilisha ile kazi ili tarehe 1 Oktoba mwaka huu kituo kianze kuhudumia wananchi” alisema Mhe. Dkt. Mpango

Akitoa salamu za mkoa wa Katavi, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mlindoko amesema Ofisi yake inaahidi kuendelea kusimamia fedha za miradi ya Sekta zote kwani fedha za Tozo ya miamala ya simu pekee mkoa ulipokea shilingi Bilioni 13.08 ambazo pia katika Sekta ya Afya zimejenga vituo vya afya sita vilivyopata shilingi milioni 500 kila kimoja ambavyo vinaendelea kukamilika.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema amepokea maelekezo ya Serikali kuhakikisha Kituo cha Afya Kibaoni kinakamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa ili kianze kutoa huduma na kuondoa kero kwa wananchi kwenda kutibiwa umbali mrefu.

“Mhe. Makamu wa Rais, tumepokea maelekezo yako kwamba ifikapo tarehe 30 mwezi wa tisa mwaka huu kituo kile kiwe kimekamilika, naomba nikuhakikishie kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI tutahakikisha tunashirikiana na Mkoa na Halmashauri kuhakikisha kituo kile kinakamilika ifikapo tarehe 30 mwezi wa tisa” alisema Mhe. Dkt. Dugange.

Mbunge wa Jimbo la Kivuu Geophrey Pinda amesema Halmashauri ya Mpimbwe ilikuwa na lengo la kupeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 589 kwa mwaka 2021/2022 kama asilimia 40 ya fedha za miradi ya maendeleo lakini hadi kufikia mwezi juni shilingi milioni 900 sawa na asilimia 166 zilipelekwa kwenye miradi mbalimbali  ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.

Akisoma taarifa ya Kituo cha Afya Kibaoni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Dkt. Martin Lohay amesema ujenzi wa kituo hicho ulianza Septemba 2021 ambapo kituo kilipokea shilingi milioni 400 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kujenga majengo matano ya wagonjwa wa nje, maabara, jengo la upasuaji, jengo la wazazi na jengo la kufulia.

Michango mingine ni pamoja na Mfuko wa Jimbo mifuko 100 yenye thamani ya shilingi milioni mbili, michango ya wananchi iliyolipa fidia ya eneo pamoja na kusogeza kokoto, mchanga na mawe na fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri shilingi milioni 100 zilizotolewa kumalizia ujenzi kutokana na changamoto ya kupungua kwa fedha za mradi kutokana na gaharama ya vitu mbalimbali.

Dkt. Lohay amesema tayari Halmashauri imepokea watumishi wapya 8 na mahitaji yao ni 52 ili waweze kutoa huduma zote kwa mara moja kituoni hapo.

Naye Bwana Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Ridhiwani Said amesema manufaa ya kituo hicho ni pamoja na wananchi kupata huduma karibu badala ya kwenda makao makuu Usevya Wilayani kutafuta huduma lakini pia kitapunguza gharama kwa wananchi ambao walifuta huduma mbali.



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.