• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Serikali yataka Wamiliki wa Shule Kuwa Wazalendo katika Utoaji wa Elimu

Imewekwa tar.: October 23rd, 2020

Na. Majid Abdulkarim, Dar es Salaam

Serikali imetoa wito kwa Wamiliki wa Shule Binafsi kuwa wazalendo katika kutoa elimu kwa kuhakikisha wanatoa elimu bora ili kuzalisha watoto wenye elimu bora itakayo wasaidia katika kulitumikia Taifa.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo jijini Dar es Salaam hapo jana katika hafla ya utoaji tuzo za kitaifa za Taaluma ya Elimu kwa walimu, wanafunzi, shule, halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri kitaaluma kwa mwaka 2019 ambapo jumla ya tuzo 485 zimetolewa kwa washindi.

Waziri Jafo amesema kuwa utoaji wa tuzo unaleta ushindani mkubwa katika shule binafsi na Umma hivyo wamiliki wa shule wanatakiwa kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania na kuacha kutanguliza maslai yao mbele bali uzalendo ili kupata watoto wenye elimu bora itakayowasaidia katika kulitumikia Taifa na kuleta maendeleo kwa ujumla.

“Utamaduni wa Utoaji tuzo utasaidia sana kuwaondoa watu wajanja ambao wanatupeleka pabaya ambapo sio muelekeo wa Taifa letu, mwelekeo wetu ni sisi wenyewe kujenga Taifa letu wenyewe kwa uzalendo mkubwa na wala hakuna mtu atakaye kuja kutoka nje kutujengea Taifa letu hata siku moja”, amesisitiza Mhe. Jafo

Aidha, Jafo amesema kuwa mwaka 2020 shule 10 bora za Kidato cha sita ni shule za nane za Umma ambapo shule tatu ni za kata huku shule iliyoongoza kitaifa ni Kisimiri, Mwandeti na Dareda.

“Hii ndiyo kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyotutuma sisi wasaidizi wake kufanya ya kuzalisha watoto bora kutoka katika shule za binafsi na umma watakaokuwa na moyo wa uzalendo wa kutumikia Taifa”

Vile vile, Mhe. Jafo ametoa pongezi kwa watendaji wote wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kazi nzuri iliyofanyika na wanayoendelea kufanya katika kuwatumikia watanzania ili kuwaletea maendeleo.

Naye Mmoja wa wanafunzi waliopata tuzo kutoka shule ya Kibaha, Alex Joseph amesema kuwa kitendo cha TAMISEMI kutoa tuzo hizo kinatoa hamasa kubwa kwa walimu, wazazi, wanafunzi  na Viongozi kwenye sekta muhimu  ya elimu ambayo ndio chachu ya maendeleo ya nchi.

“Hivyo natoa wito kwa kwa TAMISEMI kuendelea kutoa tuzo hizo kwani zinahamasisha wanafunzi wengi kufanya vizuri na kuendelea kujituma katika masomo yao” alisisitiza mwanafunzi Alex Joseph.



Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • MEWAKA KUONGEZA UJUZI WA WALIMU WETU NCHINI

    May 13, 2022
  • Halmashauri 144 zanufaika na MEWAKA

    May 13, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.