Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali Yataka Wadau Kutumia Takwimu Sahihi

Imewekwa tar.: September 25th, 2018

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewataka baadhi ya Wadau kuacha kutoa takwimu za uongo hali wakipotosha Umma kwa kuwa zipo Mamlaka kisheria zinazotoa takwimu sahii za Taifa na kwamba atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

Prof Ndalichako ameyasema hayo Jijini Dodoma leo wakati akifungua Mkutano wa pamoja wa mwaka kwa Wadau wa Mapitio ya Sekta ya Elimu nchini na kuwataka Wadau hao kuacha mara moja kupotosha jamii kupitia takwimu zisizo halisi.

Ndalichako amesema kuwa Sekta ya Elimu ni kipaumbele cha Serikali na ndio maana ruzuku ya elimu imetolewa kwa asilimia 100 na nyongeza juu yake, haiwezekani baadhi ya Wadau waseme bajeti ya elimu imeshuka kwa asilimia 56 wakati mpaka mwezi Juni, 2018 Serikali imepeleka fedha kufikia asilimia 86.5

Amesema Sekta ya Elimu imekuwa ikiimarika siku hadi siku kwani Serikali imeweza kupanga walimu kulingana na mahitaji, kujenga shule mpya, mafunzo ya walimu kazini, kujengewa uwezo kwa Wathibiti Ubora ili kuimarisha ufundishaji mashuleni ambapo jumla ya magari 45 yamenunuliwa na pia Waratibu Elimu Kata wamepatiwa pikipiki 2400 ili kufuatilia masuala ya elimu katika maeneo yao.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula, akitoa neno kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe kabla ya ufunguzi huo, amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI inafanya jitihada za kupanua utoaji wa elimu bora katika ngazi ya elimu ya msingi nchini ili kuwawezesha Watanzania wote kupata elimu.

Dkt. Chaula amesema pia Serikali inatoa fedha za matumizi ya fidia kwa ajili ya Mpango wa Elimu Bila Malipo ambapo kila mwezi zinatolewa shilingi bilioni 22.2

“ili kugharamia elimu ya msingi Bila Malipo shilingi Bilioni 22.2 zinapelekwa mashuleni kila mwezi kwa ajili ya uendeshaji wa mashule, kufidia gharama za Elimu Bila Malipo ili kuimarisha upatikanaji wa elimu kwa Wasiojiweza, wasichana, yatima na makundi mengine ya wahitaji” alisema Chaula.

Chaula amesema kutoka mwaka 2015 hadi 2018 Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maedneleo imetumia jumla ya shilingi 135,388,615,990.84 za Kitanzania kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya shule za msingi na sekondari kupitia Programu mbili za EQUIP – T na EP4R ili kuboresha elimu nchini.

Aidha Serikali imefanya uboreshaji na ukuzaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya sayansi kwa kuajiri walimu wa sayansi na hesabu wapatao 5,628 kwa shule za sekondari lakini pia walimu 7,578 wa shule za msingi wameajiriwa ili kukabiliana na uhaba uliojitokeza.

Dkt. Zainab Chaula amesema kwa kuwa mazingira ya elimu na ajira yanabadilika na yataendelea kubadilika, mjadala wa pamoja kwa wadau wa elimu utazingatia namna ya kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na wanafunzi ili waweze kupata ujuzi unaotakiwa.

Mkutano huo wenye ujumbe wa “Kutoa Elimu Bora Kwa Tanzania ya Viwanda” unalengo la kufanya mapitio ya Sekta ya Elimu kwa Pamoja, kufanya majadiliano kwa kina kwa mambo muhimu yatakayojitokeza kama changamoto na kuweka mipango na mikakati ya namna ya kukabiliana nayo.


Anaandika Fred Kibano - Ofisi ya Rais TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.