Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali yapongeza ujenzi wa madarasa mkoa wa Geita

Imewekwa tar.: December 18th, 2021

Na Fred Kibano, Geita

Serikali imeridhika na ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari mkoani Geita baada ya kukagua na kuona ujenzi kwa baadhi ya Halmashauri kufikia 95.


Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange wakati akikagua ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari za Lwezera, Bugando, Bugulula, Lutozo za wilaya ya Geita na shule za Shantamine na Geita sekondari pia baadhi ya mabweni yaliyopo Halmashauri ya Mji wa Geita.

Dkt. Dugange amesema Serikali imefanya kazi kubwa kwani kwa mkoa wa Geita pekee jumla ya shilingi Bilioni 17 na milioni 40 zilitolewa kwa ajili ya kujenga madarasa 742, vituo shikizi 102 na mabweni mawili ya wanafunzi.

“kwa mkoa wa Geita, ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari pamoja na mabweni kupitia Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko -19 zimetolewa shilingi Bilioni 17 na milioni 40”

Amezitaka Halmashauri za mkoa wa Geita, kukamilisha ujenzi wa madarasa kabla ya tarehe 30 Desemba, 2021 ikiwa ni pamoja na kuweka madawati kwenye madarasa Ili wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza kuanza masoma mapema mwezi januari 2022, lengo ni kuwa wanafunzi kuanza masomo siku moja badala ya kuwa na machaguo la kwanza la pili na la tatu.

Amezipongeza Halmashauri ya Wilaya Geita na Halmashauri ya Mji Geita kwa kutekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo Halmashauri ya wilaya ya Geita asilimia 85 na Halmashauri ya Mji Geita asilimia 95.

Akiwa katika sekondari ya Geita amesifu kazi nzuri ya mabweni na madarasa inayoendelea lakini ameagiza kukamilisha kazi hiyo kabla ya tarehe 30 Desemba mwaka 2021.

“kwa madarasa yaliyopata ajali ya moto na maabara mbili, Mkurugenzi utoe shilingi milioni 47 ili kukamilisha ujenzi kabla ya wanafunzi hawajaanza masomo mwezi januari, 2022” alisema Dkt. Dugange.

Dkt. Dugange ametoa maelekezo kwa mkoa kuongeza kasi ya ujenzi na kusimamia kasi ya ukamilishaji wa ujenzi ambao ni wastani wa asilimia 67 kimkoa inayotokana na baadhi ya Halmashauri kuchelewa ujenzi wa madarasa kutokana na sababu mbalimbali

Awali akisoma taarifa kwa Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa mkoa amesema jumla ya wanafunzi 41,822 walifaulu mtihani wa darasa la saba ambao ni sawa na asilimia 79.21 ya wanafunzi 52,797 ya waliofanya mtihani mwaka 2021.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Wilson Shimo amesema watafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kazi ya ujenzi wa madarasa inakamilika lakini pia marekebisho yote ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi ikiwemo kurudia utengenezaji wa madawati kwa kiwango kinachokubalika unakamilika kwa wakati.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.