Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali Yakabidhi hundi za Bilioni 2.3 kwa Vijiji 8 vinavyofanya biashara ya hewa ya Ukaa Tanganyika

Imewekwa tar.: July 24th, 2022

Na Fred Kibano, Tanganyika - Katavi

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekabidhi mfano wa hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3 kwa vijiji nane katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa kufanya biashara ya hewa ya ukaa.

Mhe. Mpango amekabidhi mfano wa hundi hizo katika kijiji cha Katuma Halmashauri ya Tanganyika mapema leo na kuwaasa mikoa mingine kuiga mfano wa Halmashauri hiyo ili waweze kunufaika kiuchumi na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amewataka Watanzania kupanda miti kwa wingi na kuhifadhi misitu ili kupunguza hewa ya ukaa na kuongeza upatikanaji wa hewa safi lakini pia watakuwa wanafanya biashara ya hewa ya ukaa inayohimizwa na Jumuiya ya Kimataifa.

“tumekuwa na mikataba ya Kimataifa ambayo inahamasisha biashara ya hewa ya ukaa Duniani na hii inamaana kwamba tunapopanda miti na kuhifadhi misitu ambayo inatusaidia kufyonza na kupunguza hewa ya ukaa hewani tunalipwa, hii ndiyo kwa kifupi biashara ya hewa ya ukaa” alisema Dkt. Mpango.

Aidha, amemwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kutoa elimu nchi nzima kuhusu biashara hiyo na kufanyia kazi mapungufu yote ya kisera na usimamizi wa biashara ya hewa ya ukaa ili wananchi waweze kunufaika zaidi.  

Mkuu wa Mkoa Katavi Mwanamvua Mlindoko amesema mkoa wa Katavi unayo misitu mikubwa 9, misitu 31 ya vijiji ambapo eneo lote la hifadhi ya misitu inayo takribani hekta 155,462 ambazo zinasaidia kuleta hali nzuri ya hewa na mvua. Pia ameahidi kusimamia sheria, kuhakikisha misitu inatunzwa na kusimamia uvunaji unaofaa pamoja na kuhamasisha wananchi kupanda miti kwa wingi.  

Akitoa salamu za Wizara, Mhe. Dkt. Festo Dugange Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema Ofisi yake imezipokea changamoto za usafiri kwa Wakuu wa Wilaya za Tanganyika, Mlele na Mpanda na ameahidi kuzifanyia kazi ili Viongozi hao wawe na usafiri wa uhakika.

Kwa upande wake Mbunge wa Mpanda vijijini Mhe. Suleiman Kakoso ameiomba Serikali kutatua changamoto ya kuchukuliwa msitu waliokuwa wakiusimamia ambao wamepewa Taasisi ya TAWA wanaoshindwa kuusimamia msitu huo.

Akisoma taarifa ya Mradi wa Biashara ya hewa ya ukaa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Shaban Juma amesema Halmashauri yake inatarajia kupokea shilingi Bilioni 2.3, ambazo ni fedha zilizopatikana kipindi cha kuanzia Novemba, 2021 ikihusisha vijiji nane vya Lugomesi, Mwese, Lwega, Bujombe, Kapanga, Katuma, Mpembe na Kaguma.

Aidha, amesema mradi unahusisha misitu ya vijiji vyenye eneo la hekta 216,944 za ardhi na wakazi wapatao 34,242 wanaonufaika na mradi. Pia vijiji vitapata shilingi Bilioni mbili na milioni sabini sawa na asilimia 90 na Halmashauri ya Tanganyika shilingi milioni 230 sawa na asilimia 10.

Amesema pamoja na mafanikio ya mradi zipo changamoto kama uvamizi wa maeneo ya hifadhi, uchomaji moto, ukataji miti, uchungaji mifugo na uendeshaji shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi kama kilimo cha kuhamahama.

Biashara ya hewa ya ukaa ilianza rasmi mwaka 2018 na Halmashauri ya Tanganyika na Taasisi ya Carbon Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Tuungane ambapo mapato ya biashara hiyo yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka.



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.