Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Serikali Kuajiri Wakaguzi wa Ndani 100

Imewekwa tar.: June 20th, 2019

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (Mb) amesema TAMISEMI imewasilisha maombi ya kupata kibali cha ajira ya Wakaguzi wa Ndani 100 ili kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa Kada hii katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mhe. Kandege ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kazi wa Wakaguzi wa Ndani unaofanyika kwa siku mbili katika chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Kandege amesema Wakaguzi wa Ndani ni watu muhimu, Serikali inawaamini na inatambua mchango wao  katika usimamizi wa fedha na Uwajibikaji hivyo ni vyema rasilimali watu ikawa ya kutosha ili kazi hii iweze kufanyika kwa ufanisi.

“Napenda mfahamu kuwa Wakaguzi wa Ndani ndio Jicho la Kwanza la Serikali bila  ninyi Serikali haiwezi kuona vitu ambavyo vinavyotokea kwenye matumizi ya Fedha; Mmekua mkituonyesha yale yote yanayotendeka kinyume na matumizi stahiki yaliyoelekezwa hivyo ajira hiyo itakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa kada hii” Alisema Kandege.

Akizungumzia changamoto ya Ufinyu wa bajeti kwa vitengo vya ukaguziamesema  Serikali imeongeza bajeti za vitengo vya ukaguzi kutokaa shilingi 5.6 bilioni kwa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia shilingi 6.4 bilioni kwa mwaka wa fedha 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 14.3.

“Ili kuleta tija na matokeo tarajiwa katika vitengo hivi Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya rasilimali fedha ili muweze kujitegemea katika kutimiza majukumu yenu badala ya kutegemea fedha kwa wakaguliwa” Alisema Kandege.

Wakati huo huo Mhe. Kandege ameagiza Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani kuhakikisha mianya yote ya ubadhilifu inabainishwa na kudhibitiwa kwenye mifumo ya kukusanyia mapato na usimamizi wa fedha.

Pia aliziagiza Halmashauri zote kuhakikisha Hoja zote za CAG zinapatiwa majibu, kuhakikiwa na kufungwa, ushirikiano unatolewa kwa CAG na taratibu za kufunga hoja zinazingatiwa.

Halkadhalika  Mhe. Kandege alimpongeza aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Ndugu Mohamed A. Mtonga kwa kustaafu utumishi wa umma na kazi kubwa aliyoifanya katika kada hii ya ukaguzi.

“Ndugu Mohamed nakutakia Afya njema, naamini bado una nguvu za kuendelea kutoa mchango wako kwenye shughuli za kiuchumi za kujenga Taifa letu endelea kuwa Mwalimu kiongozi kwa wakaguzi wa ndani, ukiendelea kuwafundisha na kutoa ushauri, nakutakia kila la Kheri.  Alisema Kandege.

Akizungumza wakati wa Mkutano huo Karibu Mkuu OR-TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga amesema  kutokana na umuhimu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani fedha zilizotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya Kitengo hiki zitalindwa na kuhakikisha zinatumika kwa ajili ya kazi za kitengo hiki pekee.

“Umefika muda sasa vitengo vya wakaguzi wa ndani kuimarishwa na Kila Mkoa na Halmashauri kuviwezesha vitengo hivi rasilimali fedha, watu na vitendea kazi vya kutosha wakati wote” Alisema Nyamhanga.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ukaguzi na Ufuatiliaji Ofisi ya Rais TAMISEMI Miriam Mbanga amesema Mkutano wa kazi kwa wakaguzi wa ndani wa Mikoa na Halmashauri wa kwanza kufanyika na unalenga kujifunza, kubadilishana uzoefu, kushirikishana namna mbalimbali ya kutatua changamoto za kiukaguzi na kujiwekea malengo ya namna ya kufanya kazi ya ukaguzi wa ufanisi.

Mkutano huu umehudhuriwa na Wakaguzi wa Ndani zaidi ya mia moja na hamsini kutoka katika Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.  


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.