Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Sera ya Taifa ya Ugatuaji Kuiwanua Wananchi Kiuchumi

Imewekwa tar.: February 3rd, 2020

Serikali inaandaa Sera ya Taifa ya Ugatuaji ambayo itasaidia kuandaa sheria ambayo itamairisha utendaji wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kukuza uchumi wa jamii, kuboresha utawala bora na ushiriki wa jamii katika masuala ya sekta mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa morogoro, Mhe. Loata Sanare wakati akifungua warsha ya kukusanya maoni ya wadau katika kuandaa Programu ya Kuimarisha Mikoa na Serikali za Mitaa (Regional and Local Government Strengthening Programme-RLGSP) katika Manispaa ya Morogoro.

“Sera hiyo inakusudia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini, kuzalisha ajira na ustawi wa jamii, Kuimarisha mfumo wa Ushirikishwaji wa wananchi kijamii, kisiasa na usimamizi wa Uchumi”

Pia Sanare amesema uboreshaji wa uhusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika kutoa huduma zilizogatuliwa, Usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya Tabianchi, Usawa wa  Kijinsia, Maendeleo mijini na vijijini, Usalama wa chakula na lishe na makundi yenye mahitaji maalum.

Akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa warsha Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameishukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuanzisha Sera ya Taifa ya Ugatuaji inayotolewa maoni kwa lengo la kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi kwa wakati na ufanisi.  

Kwa upande wake Mhandisi Enock Nyanda Mkurugenzi Msaidi Idara ya Uratibu wa Sekta Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema mbali na kuwepo Mpango wa Maboresho wa kwanza na wa pili, awamu hii kutakuwa na Sera ya Taifa ya Ugatuaji itakayosimamiwa na sheria ambayo itaonyesha ushiriki wa Wadau mbalimbali na itasaidia kutatua changamoto zilizopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Programu hiyo ni mwendelezo wa mambo mazuri yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa Programu za Maboresho ya Serikali za Mitaa zilizotangulia  Awamu ya kwanza na ya pili (LGRP I & II) zilizotekelezwa kati ya mwaka 2000 hadi 2010.

Sera ya Taifa ya Ugatuaji pamoja na  mkakati wake wa utekelezaji umeainisha nguzo kuu 9 ambazo baadhi yake zinalenga kutoa mwongozo kuhusu ukusanyaji na usimamizi wa Rasilimali fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutekeleza wajibu wa utoaji huduma kwa mujibu wa sheria, Kuinua na kuimarisha Uratibu wa jitihada za kuendeleza Uchumi wa Maeneo (Local Economic Development) katika ngazi za msingi kwenye Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Programu inatarajiwa kutekelezwa kwenye ngazi za Sekretariati za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kipindi cha miaka 10 kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ikiwa na lengo la kuona wananchi wanapata huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa kufanya mageuzi ya uendeshaji na uwajibikaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI itafanya uratibu wa utekelezaji wa programu hiyo.

Washiriki katika warsha hiyo ni pamoja na baadhi ya Wakurugenzi na wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala wasaidizi wa Seksheni ya Serikali za Mitaa, Wataalam kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

          Anaandika Fred Kibano




Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.