Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KULETA SERIKALI KWA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO - MHE. MCHENGERWA

Imewekwa tar.: May 3rd, 2025

Na John Mapepele

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imedhamiria kwa dhati kuisogeza Serikali karibu zaidi na wananchi wake hasa wale walio na kipato cha chini katika maeneo ya vijijini na mijini ili kuwaletea maendeleo.

Akizungumza kwenye Kongamano la Uchumi la Arusha  leo Mei 3, 2025 jijini Arusha akiwa miongoni mwa watoa mada, Mhe. Mchengerwa amefafanua kwamba lengo kuu ni kuwakomboa wananchi kutoka katika mnyororo wa ukosefu wa taarifa, huduma na fursa, kwa kuwajengea uelewa, uwezo na maarifa ya msingi, sambamba na kuwawekea miundombinu inayowawezesha kushiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mipango yao ya maendeleo.

“Tupo katika zama ambazo maendeleo hayategemei tena maamuzi ya viongozi wa kitaifa peke yao, bali yanategemea uwezo wa maeneo yetu ya mikoa na halmashauri zetu kuongoza kwa dira, maarifa na maamuzi ya kimkakati”.Amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha, amesema utawala bora siyo tu matumizi ya sheria bali ni falsafa ya kuwezesha kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika ndoto ya taifa na kujenga taasisi imara, kusimamia rasilimali kwa uadilifu, na kutoa huduma kwa usawa bila upendeleo.

Amesisitiza kuwa kwa kutumia sera ya Decentralization by Devolution (D-by-D), halmashauri zimewezeshwa kupanga na kutekeleza mipango yao kulingana na vipaumbele vya wananchi wao na kwamba hiyo ndio njia ya kweli ya kukuza demokrasia ya kiuchumi. 

”Kwa maana hiyo, TAMISEMI imewapa halmashauri zetu nguvu ya kufanya maamuzi kwa mujibu wa mazingira ya jamii zao. Hili linawezesha uwekezaji wa ardhi, huduma bora kwa wananchi, na kuimarisha mapato ya ndani”. Ameongeza Waziri Mchengerwa

Akifafanua zaidi amesema ustawi wa mikoa hautatokana na maazimio ya makaratasi pekee, bali na uthubutu wa viongozi wake kuondoa matabaka baina ya walionacho na wasio nacho ambapo amesisitiza mikoa ina wajibu wa kufanya tafiti za kina za fursa zilizopo, kutambua changamoto kisekta, kutafuta majawabu yanayotekelezeka na kuanzisha ubia mtambuka (multi-sectoral partnerships) kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Waziri Mchengerwa ameagiza kwamba  kongamano lisiwe tu mkutano wa mijadala, bali chemchemi ya fikra mpya, dira ya uwekezaji wenye tija, na mlango wa fursa kwa kila raia wa Mkoa wa Arusha  iwe ni kijijini au mijini. 

Ametaka  ongamano hilo liwe chachu ya kufungua milango mipya ya uwekezaji kwa kushirikisha Wizara na Taasisi zote husika za Serikali ili kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji yanaboreshwa  kwa wepesi, uwazi na ushawishi chanya. 

Maeneo yaliyotambuliwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya uwekezaji yaharakishwe kuhuishwa kwa kupangwa kitaalamu, kupimwa kwa usahihi, fidia zote itolewe kwa haki, na miundombinu ya msingi (barabara, maji, umeme, mawasiliano na huduma nyingine) ijengwe kwa haraka. 

Amesisitiza kuwa wananchi na wadau wa sekta mbalimbali washirikishwe kwa kina, kwa uwazi, na kwa heshima  pasipo ubaguzi wa hali za kiuchumi, jinsia, mila wala hadhi ya mtu. 

Pia mchango wa wananchi wa kawaida unaojumuisha wakulima, wafanyabiashara wadogo, vijana na wanawake lazima uwekwe kikamilifu kwenye mpango unaotokana na Kongamano hili. 

Aidha, ameelekeza sheria za nchi zisimamiwe kwa haki, weledi na uadilifu ili kulinda rasilimali za Mkoa na taifa na kwamba  tusiruhusu migogoro isiyo ya lazima ififishe ndoto za mamilioni bali, tutumie maarifa ya ndani na teknolojia ya kisasa, kujifunza kutoka kwa uzoefu wa ndani na nje ya nchi, ili kubuni uwekezaji wa kisasa wenye tija na ustahimilivu wa muda mrefu.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • WAACHENI WATOTO WAENDE SHULE- RAIS SAMIA

    June 16, 2025
  • NIMESAINI NOTISI ZA KUVUNJA MABARAZA YA MADIWANI - MCHENGERWA

    June 15, 2025
  • MANYARA BINGWA RIADHA WASICHANA NA WAVULANA MITA 1,500

    June 15, 2025
  • MHE MCHENGERWA AWATAKA MA RC, DC KUONGOZA JOGGING KWENYE MAENEO YAO

    June 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.