• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Pawaga Atoa Wosia Mzito kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI

Imewekwa tar.: May 18th, 2018


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) aliyemaliza muda wake katika Utumishi wa Umma Mohammed Pawaga amewataka watumishi wote wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia utu.

Pawaga ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na watumishi wa idara, vitengo na Taasisi mbalimbali wa Ofisi ya Rais TAMISEMI iliyofanyika ndani ya ofisi hiyo.
Mbali na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia kufika hatua hiyo ya kustaafu kwa heshima lakini pia aliwaasa watumishi kutumia vyeo na madaraka yao katika kutatua changamoto za kazi kwa weledi.

“Kila mtu awe na ndoto ya kufika hapa, namshukru Mwenyezi Mungu kwa miaka 35 kuwa kazini kwani katika maisha kuna mambo mawili ambayo hayaepukiki ambayo ni kustaafu pamoja na kifo” Alisema Pawaga na kuongeza,

“Mambo haya yote yanahitaji maandalizi, kustaafu unatakiwa ujiandae mapema, kwamba kile ulichokipata unakitumiaje baadaye, na kifo unatakiwa ujiandae kwa matendo mema, nafurahi kuona nastaafu kwa amani” Alisema.

Alisema kiongozi yeyote anatakiwa kutengeneza viongozi na siyo wafuasi hata pale kunapotokea kutokuelewana inapaswa kutatua changamoto hiyo kwa kuzingatia utu jambo ambalo litakuongezea ujuzi na mafunzo katika utendaji wa kazi.

Aliwataka watumishi hao kutobadilika tabia baada ya kupata madaraka au pesa, kwani alisema vitu hivyo humbadilisha binadamu hivyo kuwashauri wale wenye vyeo kukumbuka walipotoka kabla ya kufanya maamuzi ili waweze kuwasaidia kila mmoja kwa kadiri wanavyoweza.

Akitoa salamu za pongezi za idara ya utawala na rasilimali watu mkurugenzi msaidizi wa utawala Mrisho Mrisho amempongeza Bw Pawaga kwa kuikuza TAMISEMI katika nyanja mbalimbali kama vile kuongeza vitengo, watumishi, upanuzi na ukarabati wa majengo pamoja na kuwepo kwa mazingira bora na rafiki ya kazi.

“Tunajivunia kuwa na wewe kwa miaka kumi uliyokaa hapa kwa sababu umechangia kuikuza TAMISEMI, ilikuwa chini na sasa ipo juu, umeanzisha vitengo vipya pamoja na taasisi mbalimbali sambamba na kuongeza idadi kwa watumishi” Alisema Mrisho

Mrisho amesema awali kulikuwa na watumishi 270 lakini kwa sasa wapo watumishi 658, lakini mbali na wingi huo lakini amesema Mkurugenzi huyo amewafundisha uwajibikaji jambo ambalo limesaidia watumishi kufanya kazi kwa umoja na kwa upendo wa hali ya juu.

Salamu kutoka Kitengo cha mawasiliano serikalini zilizotolewa na Fredy Kibano zilimuelezea Bw Pawaga kuwa ni kiongozi aliyefanikiwa kwa kiwango kikubwa kusimamia ukweli, haki na kutengeneza uwelewano ndani ya idara na vitengo vya TAMISEMI.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi Serikali Kuu TUGHE, tawi la TAMISEMI Jumbe Akida amesema kuwa Pawaga alijali stahiki za wafanyakazi bila kujali tofauti ya vyeo huku baadhi ya wawakilishi kutoka idara, vitengo na Taasisi mbalimbali zikimuelezea kama mtu aliyejali watu wote bila kuangalia umri wala madaraka.

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • MEWAKA KUONGEZA UJUZI WA WALIMU WETU NCHINI

    May 13, 2022
  • Halmashauri 144 zanufaika na MEWAKA

    May 13, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.