Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Ondoeni vikwazo ujenzi Miradi ya Maendeleo – Prof Shemdoe

Imewekwa tar.: September 6th, 2021

Na Fred Kibano na Mathew Kwembe, Kilosa

Serikali imeagiza kuharakisha ujenzi wa vituo viwili vya afya vilivyopatiwa fedha mwaka huu 2021/2022 kiasi cha shilingi milioni mia tano pamoja na shule ya sekondari iliyopatiwa shilingi Bilioni moja mara ifikapo mwezi Desemba mwaka huu

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe wakati wa ziara yake Wilayani Kilosa hii leo.

Akiongea na watumishi wa kada mbalimbali katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Ilonga Prof. Shemdoe amesema kumekuwepo na malumbano ya muda mrefu juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari iliyotolewa fedha shilingi Bilioni moja kutoka Serikali kuu na vituo viwili vya afya vilivyopatiwa fedha mwaka huu ambapo ujenzi wake bado haujaanza kutokana na sababu zisizo na msingi kama vile mchakato wa manunuzi.

“Ninamasikitiko kidogo Kilosa, tumeleta hapa fedha shilingi Bilioni moja kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari , mmevutana sana  mpaka leo kazi haijaanza, Katibu Tawala Mkoa nakuomba hili ulisimamia kwa karibu mpaka Desemba tuje tuone progress (maendeleo) nzuri  shilingi Bilioni moja ipo kwenu imeshindwa kutumika. Tumeleta shilingi milioni mia tano kwa vituo viwili vya afya hilo na lenyewe lianze kufanyiwa kazi” alisema Shemdoe.

Aidha katika mwaka huu wa fedha amesema viomeongezwa vituo vya afya viwili kwa kuwa Halmashauri hiyo inayo majimbo mawili ya uchaguzi ambapo ameagiza fedha hizo shilingi Bilioni moja zianze kutumika mara moja ili huduma stahiki ziweze kutolewa kwa wananchi.

Amesema kero kubwa ambazo waliziwasilisha kwake ya uhaba wa watumishi kama Mhandisi na Mkaguzi wa ndani tayari wameshapelekwa na kwa sasa anaiangalia upya ofisi ya manunuzi kwa kuwa wanaonekana kama wanakwamisha michakato ya manunuzi wilayani humo.

Katika hatua nyingine Shemdoe amewataka Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa kusaidia kazi za ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi na pia kama sehemu ya utawala bora pamoja na kuzingatia (force account) nguvu kazi ya jamii

Amekemea tabia za rushwa kwenye Halmashauri hiyo zinazofanywa na baadhi ya Maafisa ambapo barua zilizopitishwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI zimekuwa zikitozwa kwa shilingi laki tano jambo ambalo alidokezwa na baadhi ya watumishi walioomba uhamisho wilayani hapo na kusisitiza kwamba jambo hilo halivumiliki na sheria zitachukuamkondo wake.  

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Ntunguja amemshukuru Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kwa kupokea kero na ushauri wa watumishi pamoja na kujibu kero zao.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kilosa Bw. Kisena Mabuba amesema ukusanyaji wa mapato ya ndani katika halmashauri hiyo 2020/2021 ulikuwa ni asilimia 84 na kwa mwaka huu makusanyo wanatarajia kukusanya kwa asilimia 100 ijapokuwa hadi sasa makusanyo ya mwaka 2021/2022 ni asilimia pekee.  


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NENDENI MKAITANGAZE SERIKALI.

    May 24, 2025
  • SOKO LA KISASA LA NYAMA CHOMA LAZINDULIWA VINGUNGUTI

    May 24, 2025
  • DKT. Biteko asisitiza wazazi kuthamini nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya mtoto.

    May 24, 2025
  • Mhe. Rais Samia amtaka Prof. Nagu kuboresha  huduma ya afya ya msingi.

    May 24, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.