• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

NDEJEMBI ATAKA UENDELEVU MFUMO WA M-MAMA

Imewekwa tar.: May 17th, 2023

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Mhe.  Deogratius Ndejembi amewataka waratibu wa Mfumo wa Usafirishaji wa Dharula kwa akina mama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga(m-mama) kuwa endelevu. 

Ndejembo ameyasema hayo leo Mei 16, 2023 wakati wa kufungua kikao kazi cha waratibu wanao simamia mfumo wa m-mama kilichofanyika jijini Dodoma..

Amesema  Serikali imeleta mfumo huo ili kutatua changamoto ya rufaa na usafiri wa dharura kwa wamama wajawazito, waliojifungua na watoto hapa nchini.

“Bado tuna changamoto kubwa kwenye usafiri wa dharura, na jambo hili ni moja ya vipaumbele katika kuokoa maisha ya Wajawazito na watoto wachanga wanapokuwa na dharura za kiafya na ndio maana imekuja na mfumo huu.”amesema Ndejembi

Ndejembi pia amehimiza ushirikiano  kwa wadau wote wanaohusika katika kuutekeleza mfumo wa m-mama na kuhakikisha gharama za usafiri wa dharura kwa akina mama wajawazito, waliojifungua na Watoto Wachanga zimejumuishwa katika mipango na bajeti kwa kila halmashauri. 

Pia amewataka kufuatilia watendaji wa vijiji na kuwaelekeza kuwatambua wamiliki wa magari vijijini, kuwasajili na baadaye halmashauri kuingia nao makubaliano.

Ndejembi amewaagiza waratibu hao kuhakikisha wanafuatilia malipo ya madereva ili walipwe kwa wakati na kuweza kutoa huduma bora kwa jamii. 

“Hakikisheni hawa wanajamii wanalipwa kwa wakati. Madereva jamii hawa wakilipwa kwa wakati, watakuwa vinara  wazuri sana kwenye mfumo huu, wataumiliki mfumo na kuhakikisha unatekeleza vizuri, hivyo fuatilieni wasije wakaandamana huko.”amesisitiza

Naye Mkuu wa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya Zanzibar  Mahamed  Mafazy amesema

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejipanga kuanzisha mfuko ambao utamlazimisha mwananchi kuwa na bima ya afya na kuifanya huduma ya magari ya wagonjwa kufanywa na sekta binafsi huku mfumo wa M-Mama ukipewa kipaumbele.

“Mbali na hatua ya Serikali kununua magari ya wagonjwa 11 kwa kila wilaya, pia tutatoa fursa kwa sekta binafsi kutoa huduma hii na tutazisajili gari hizo ili zitoe huduma kwa wananchi.”amesema Mafary

Kwa upande wa Meneja wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Joseph Sayi amesema katika kutekeleza mfumo huo mpaka sasa  safari 21,000 zimefanyika na kuokoa maisha ya watoto wachanga na akina mama zaidi ya 805.

“Haya ni mafanikio makubwa ambayo yasingewezekana bila juhudi zetu sote ”

Amesema ili kufanikisha usambazaji wa Mfumo wa m-mama nchini Vodacom kupitia Foundation yake imetoa dola za Marekani milioni 10 na shirika la USAID limetoa dola za Marekani milioni 5 wakati Serikali ya Tanzanioa imechukua jukumu la kulipa madereva jamii na kuchukua gharama za rasilimali watu kataka Wizara zake za afya na TAMISEMI.

Mratibu wa Mfumo wa M-Mama Taifa Dkt. Yahaya Hussein Kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI amesema mfumo huo unatekelezwa katika mikoa 14 ya Tanzania Bara na Mikoa yote ya Zanzibar


Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA - UALIMU NA AFYA - TAMISEMI APRILI, 2023 April 12, 2023
  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI HAJARIDHISHWA USIMAMUZI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA CHEMBA - DODOMA

    May 31, 2023
  • MIKATABA YA UTEKELEZAJI MRADI WA UENDELEZAJI WA JIJI LA DAR ES SALAAM DMDP 2 YASAINIWA

    May 30, 2023
  • DKT. MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA ALAT

    May 30, 2023
  • WANANCHI KIJIJI CHA MAJALILA WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE

    May 23, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.