Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Naibu Waziri ataka majengo ya hospitali Gairo yakamilike kwa wakati

Imewekwa tar.: June 21st, 2021


Na Mwandishi wetu, Morogoro

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo John Dugange amewaagiza Viongozi wakuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo kwani inatakiwa kukamilika katika muda uliopangwa.

Mhe Dkt Dugange ametoa agizo hilo Juni 20, mwaka huu wakati alipokutana na Viongozi wa Wilaya, Watendaji wa Halmashauri pamoja na watumishi wa Idara ya Afya wakati akikagua ujenzi wa majengo saba ya Hospitali ya Wilaya ya Gairo na ujenzi wa boma kwenye zahanati ya Mogohigwa iliyopo kata ya Chigela.

“Nakuagiza Mkurugenzi ukishirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri, hebu kasimamieni kwa ukaribu miradi yote na mhakikishe inakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma tulizo kusudia hususani kwa hii miradi ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na zahanati mpya ya Mogohigwa, lakini pia hata kwa miradi ya urekebishaji miundo mbinu kwenye zahanati za zamani,” amesema.

Amefafanua kuwa ni lazima pawepo na usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya kupitia miradi ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya, uboreshaji wa miundominu kwenye kituo cha afya na zahanati pamoja na ujenzi wa zahanati mpya ili thamani ya pesa ilingane na ubora wa majengo yaliyopo na miundo mbinu mingine.

"Mkurugenzi hili nalo ni muhimu sana kulizingatia, Serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya sekta ya afya, lengo ni kuhakikisha Wananchi wake wananufaika na ubora wa huduma, hivyo thamani na ubora wa majengo pamoja na miundo mbinu yake lazima ilingane kabisa na thamani ya fedha zilizotumika,” amesisitiza Naibu Waziri.

Dkt Dugange amesifu kasi ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na kueleza kuwa juhudi za Halmashauri zinaonekana ingawa kulikuwa na kasoro ndogondogo ambapo alielekeza kasoro hizo zirekebishwe haraka katika kipindi cha mwezi mmoja ili huduma zianze kutolewa hususani jengo la maabara ifikapo Julai 20, 2021.

“Umaliziaji siyo mzuri sana, nadhani kulikuwa na shida katika usimamizi kwa mafundi mliowapa kazi hii na hapa jicho langu lipo kwa Mkurugenzi kama msimamizi Mkuu, Mganga Mkuu Wilaya na Mhandisi wa ujenzi mmeonyesha udhaifu, ingawa ninawapongeza kwa kasi nzuri ya ujenzi na majengo ni mazuri lakini umaliziaji wake kidogo bado sijaridhishwa nao,” ameeleza.

Aidha Dkt. Dugange  amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri Bi Agnes Mkandya pamoja na Mweka Hazina Wilaya kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuhakikisha wanafikia lengo la 100% ifikapo juni 30, 2021 kabla ya mwaka mpya fedha 2021/2022 kuanza.

“Suala la makusanyo kwa Gairo bado mpo chini sana ni 67% tu ya lengo, naagiza pia lipewe uzito zaidi ili kufikia Juni 30, mfike lengo la 100%,” alisema na kuongeza:

 “Kupitia makusanyo ya ndani mtakuwa na nguvu ya kujiendesha bila kuwa na utegemezi kutoka Serikali kuu, pia itasaidia kuimarisha miundombinu katika utoaji hudumwa kwa jamii.”

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.