• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Mwakyembe afunga mashindano ya FEASSSA Arusha

Imewekwa tar.: August 24th, 2019

 Na Mathew Kwembe, Arusha

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameyafunga Mashindano ya 19 ya michezo ya shule za Sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki (FEASSSA) kwa kuahidi kuwa mwakani timu kutoka Tanzania zitaleta upinzani mkali kulinganisha na mwaka huu.

Akizungumza kwenye sherehe za kuhitimisha mashindano hayo zilizofanyika leo  leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Mhe.Mwakyembe amewatahadharisha wenyeji wa mashindano hayo mwakani nchi ya Kenya kuwa wakae tayari kwani timu kutoka Tanzania zitakuja kwenye michuano hiyo kwa kishindo.

Amesema kuwa katika mashindano ya FEASSSA mwakani ambayo yamepangwa kufanyika katika  mji wa Kakamega nchini Kenya, timu za kutoka Tanzania zitaleta upinzania mkali kwani zitakuja kwenye mashindano hayo zikiwa zimejiandaa vizuri.

“Napenda kukuhakikisha Rais wa FEASSSA kuwa tutaziandaa timu zetu vizuri ili mwakani ziweze kushinda makombe mengi,” amesema Mhe.Mwakyembe.

Aidha Mhe.Mwakyembe amezitaka timu za nchi wanachama zilizoshiriki mashindano haya kuhakikisha kuwa zinafanya maandalizi ya kutosha kwani bila hivyo zitaendelea kutofanya vizuri.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi Odilia Mushi amesema jumla ya washiriki 3600 wameshiriki mashindano ya FEASSSA, wakiwemo washiriki kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Uganda, Zanzibar,Tanzania na nchi ya Malawi walishiriki michuano hiyo kama mgeni mwalikwa.

Amesema michuano ya mwaka huu mbali na kuwashirikisha wanafunzi wa sekondari pia iliwahusisha wanafunzi wa shule za msingi, wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Bi Mushi ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha kuwa kuwa kila mwaka wawashirikishe wanafunzi walio kwenye mahitaji maalum.

“Natoa wito ushirikiano huu ambao tumeuonyesha Afrika Mashariki kwa kuuonyesha kwa wenzetu hawa wenye mahitaji maalum,” amesema.

Ameongeza kuwa michezo hii imefanyika kwa ufanisi mkubwa ambapo kila nchi ilipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao, na kuongeza kuwa changamoto zilizojitokeza mwaka huu zitakuwa kichocheo kwa ajili ya kufanya vizuri katika mashindano ya mwakani.

Naye Rais wa FEASSSA bwana Justus Mugisha amesema kuwa kuanzia mwakani jina la mashindano hayo litabadilika kutoka kuwa  FEASSSA hadi FISSA na kuongeza kuwa timu zitakazoshiriki mashindano hayo zimeongezewa siku moja zaidi ili kutoa fursa kwa wawakilishi wa kila nchi kwenda kwenye utalii wa ndani.

Aidha bwana Mugisha amezitaka nchi wanachama kuhakikisha kuwa  zinafanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kushiriki mashindano mengine ya FEASSSA kwani bila kufanya hivyo itakuwa ni ndoto kwa timu hizo kushinda michuano hiyo.

Akizungumzia michuano hiyo, bwana Mugisha amesema kuwa  mashindano ya mwaka huu yalikuwa ni magumu kulinganisha na mashindano yaliyopita na hivyo akataka timu ambazo hazikufanya vizuri mwaka huu ziende zikajiandae kwa ajili ya michuano mingine kama hiyo itakayo fanyika mwakani nchini Kenya.

Kabla ya kufunga mashindano hayo Waziri Mwakyembe alipata fursa ya kushuhudia pambano kali la fainali la mpira wa miguu baina ya timu mbili za Uganda.

 

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.