Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

MTOA HUDUMA ZA AFYA ATAKAYESABABISHA KIFO CHA MGONJWA KWA UZEMBE NITAMTENGUA ; MHE. MCHENGERWA PWANI

Imewekwa tar.: September 9th, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema, yeyote atakayeshiriki kufanya uzembe katika vituo vya afya, zahanati na hospitali nchini atachukuliwa hatua kali.

Ameyasema hayo Septemba 7,2024 katika Hospitali ya Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa na vifaa tiba kwa ajili ya huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) na watoto wachanga wagonjwa na wenye uzito pungufu.

Vifaa na vifaa tiba hivyo vimefadhiliwa na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation.

"Kila anayekwenda kupata huduma za afya kama ni kituo cha afya kama ni zahanati na kama ni hospitali za halmashauri, kila mtoa huduma aende akatoe huduma hii kwa kila Mtanzania kwa wema akimkaribisha vizuri, akimskiliza kero yake vizuri na kumuhudumia mara moja.

"Haya tumekwisha kubaliana na tumepeana mipaka kwamba yeyote atakayeshiriki kufanya uzembe, mwananchi asipate huduma vizuri ikapelekea uzembe wa kifo cha Mtanzania yeyote hospitali yoyote maana yake mganga mkuu wa wilaya, mganga mkuu wa mkoa ninawatengua kesho yake.

"Na hii tumeshakubaliana, sitarudi nyuma kwa hili, ninadhani umenisikia Dkt.Mfaume nikisikia popote Mtanzania amekwenda kupata huduma hajapata huduma vizuri nitachukua hatua.

"Nikisikia popote Mtanzania au mama mjamzito amefariki kwa uzembe au mtoto amefariki kwa uzembe kwa sababu hakuhudumiwa au hakupewa rushwa mtoa huduma kama ilivyotokea kule Kahama na maeneo mengine maana yake wahusika wote pale watakuwa hawana kazi tena, mganga mkuu wa wilaya, mganga mkuu wa mkoa ninawatengua mara moja wala sitanii.

"Na wale waliohusika katika eneo hilo tutachukua taratibu za kinidhamu, sisi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ili kuhakikisha yeyote aliyefanya uzembe mtoto akafariki, mama mjamzito akafariki awe ni daktari awe na degree moja au mbili au tatu tutakamata cheti chake.

"Hatafanya kazi tena katika nchi hii au hata akitoka nje ya mipaka ya mipaka hii hataruhusiwa kufanya kazi ya uganga au kutoa huduma katika Sekta ya Afya maana yake cheti chake kitakuwa kama pambo anaweza kupamba nyumba yake wala hatuna tabu.

"Lakini hataruhusiwa kutoa tiba ndani ya nchi hii na nje ya mipaka ya nchi hii, tutasitisha kila kitu ndiyo utaratibu na wao wanajua, wana viapo.

"Mtanzania anapokwenda kupata huduma lazima asikilizwe na lazima ahudumiwe vizuri, kwa sababu hawa ndiyo wanatufanya tuendelelee kufanya kazi bila wao wannchi hakuna nchi, bila wananchi hakuna Serikali.

"Kwa hiyo huo ndiyo ukweli kwa hiyo kila mtumishi lazima tujishushe na sitanii kwa hili, sitanii hata kidogo atakayejiingiza kwenye mtego huu kesho yake hana kazi wala sitanii.

"Kama ni mganga mkuu wa wilaya tumewapa magari, tutawany'ang'anya magari na tutawarudisha kwenye nafasi zenu za kuwa daktari wa kawaida, wala sina mchezo kwa hili awe mganga mkuu wa mkoa nitafanya hivyo hivyo.

"Na kwa sababu ni mamlaka yangu nitatengua siku inayofuata ninaweka pembeni,tunateua mtu mwingine kufanya kazi katika eneo hili kuwahudumia Watanzania hili sitanii.

"Tumeshakubaliana na Mkurugenzi wa Afya na Naibu Katibu Mkuu Afya muende mkalisimamie, kaeni na wataalamu zungumzeni nao na wale wenye changamoto kaeni mzitatue,"amefafanua Waziri Mchengerwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.