Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mikopo ya Sh. Milioni 850 yatolewa kwa Vikundi 104 jijini Tanga

Imewekwa tar.: February 15th, 2021

Na Tussa Mwambenja, Tanga

Halmashauri ya Jiji la Tanga imetoa mikopo yenye thamani ya sh.850,343,274 kwa vikundi 104 vya wanawake, vijana na walemavu ikiwa ni kutekeleza agizo la serikali kwa kila halmashauri nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Mkurugenzi wa Jiji hilo Daudi Mayeji amesema fedha hizo zimetolewa kwa Vikundi 73 vya wanawake, 25 vya vijana na 6 vya watu wenye ulemavu.

Kikundi cha Winners Women Group ni miongoni mwa vikundi 73 vilivyonufaika na mikopo hiyo kwa upande wa wanawake ambapo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kikundi hicho Fatuma Sheshe, amekiri kikundi chake kupokea kiasi cha sh. milioni 20 ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa za ujasiriamali kama ufugaji nyuki, ufugaji wa kuku, kutengeneza batiki, sabuni za maji na kikoba.

Amesema kikundi hicho chenye wanachama 30 wote wakiwa wanawake kwa sasa kina mtaji wa sh. milioni 47 unaokiwezesha kikundi kuendesha shughuli zake kwa ufanisi mkubwa huku kikiweza kurejesha shs.16,000,000 kati ya shs.20,000,000 ilizokopa na hivyo kubakia na deni la sh milioni nne tu.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuunga mkono wanawake pale tunapoonyesha juhudi kwani kwakweli tunasomesha watoto, tumeboresha biashara zetu za mtu mmoja mmoja kwasababu tumeongeza mitaji yetu,” amesema.

Kwa upande wake mweka hazina wa kikundi hicho Fatuma Mshote ameelezea furaha yake kwa kikundi chao kupata mkopo kwani umewasaidia sana kujiinua kiuchumi na akaomba serikali kuwaongezea muda wa marejesho kwani muda wa sasa ni mdogo.

Vijana ambao ndio tegemeo la Taifa nao hawakuachwa nyuma katika mikopo hii ili waweze kujenga Taifa lenye Uchumi wa kati lakini lenye nguvu na ubunifu mkubwa, tuelekee kwa Vijana wa pale Mwakidila.

Mwakidila Chapakazi Youth Group ni kikundi cha Vijana kilichoanzishwa 2015 kilichopo kata ya Tangasisi mtaa wa Mwakidila B, kikiwa na wanachama 11 wa kike wakijishughulisha na ufyatuaji wa matofali na kilimo cha matunda hususani Tikiti.

Mwakidila Chapakazi walikuwa na mtaji wa shs.5,200,000 wakakopeshwa na Halmashauri shs.10,000,000 ambazo wameziendeleza kwenye kilimo kwa kununua shamba la heka moja lililopo Chongoleani, pamoja na kuajiri vijana wenzao wengine 10 katika ufyatuaji wa matofali, Mwenyekiti wa kikundi hiki Nasibu Musa amesema mkopo walioupata umeleta mafaniko makubwa sana kwao, kwani sasa wanakikundi wana viwanja ambavyo kila mmoja amenunua kama faida yake binafsi lakini pia wanasomesha watoto na wadogo zao Sekondari.

“ Kupitia mkopo huu tumenunua shamba heka 1 Chongoleani, kwa shughuli zetu hizi tumeweza kununua viwanja na kusomesha wanetu na wadogo zetu sekondari, binafsi nikisikiaga wimbo wa Magufuli jembe uwa nafurahi sana sababu ujembe tumeuona kupitia Halmashauri yetu ya jiji maana wengi wetu tumetoka chuo tukaona tujiajiri na Maisha yanasonga,” amesema Musa

Kikundi kingine kilichonufaika na mikopo ya asilimia 10 ni TAYOTAI, hiki ni kikundi cha vijana wa kike kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za aina mbalimbali, ambacho kinapatikana kata ya Makorora eneo la Community Center kama Tanga Youth Tailoring (TAYOTAI).

Kikundi hiki ambacho kimenufaika na mkopo unaotolewa kwa vijana, kimesajiliwa 2019 kikiwa na jumla ya wanakikundi 32, na kimepata mkopo wa shs.100,000,000 ambao ulitumika kununua Vyerehani za kisasa vinavyotumia umeme na kuanzisha mtaji wa shughuli za Ushonaji kama Sare za Shule, Manesi, pia kushona nguo za mitindo mbalimbali yenye ubunifu.

“Tunapenda kuendelea kuishukuru serikali kwa mkopo waliotupatia sisi vijana wa kike ambao wengi wetu tuna umri kuanzia miaka 19 mpaka 35, tulikuwa tunakaa tu nyumbani bila shughuli yoyote ile hali iliyokuwa inatupelekea kuwa wake za watu katika umri mdogo na kuwa tegemezi kwa wazazi, lakini sasa tuna ofisi ambayo tumepewa na jiji, pia tuna ujuzi  wa kushona kwa mashine ya kudarizi ambao tumeongezewa na Serikali kupitia Halmashauri ya jiji la Tanga, kiasi tumekuwa tukipata tenda katika baadhi ya shule na vituo vya Afya kama Galanos sekondari, kituo cha Afya Duga, Mikanjuni, Makorora, na Masiwani,” alisema Fatma Amiri Katibu wa kikundi

Tanga One Youth ni miongoni pia mwa vikundi vya vijana vilivyonufaika na mikopo inayotolewa, kikundi hiki kilipata mkopo wa sh 182,000,000, mkopo ambao umetolewa kwa vijana 70 wanaojishughulisha na usafirishaji wa abiria maarufu kama “Bodaboda” ambapo fedha ya mkopo ilitumika kununua pikipiki 70 pamoja kulipia bima, kununua mafuta ya kuanzia na vibali vyote vinavyohusika.

Tanga Viziwi Group ni kikundi kimojawapo cha watu wenye ulemavu kati 6 ambacho kinapatikana Makorora, kimesajiliwa mwaka 2018 kikiwa na wanachama 8, kikijishughulisha na utengenezaji wa Samani, kupiga picha za mnato na ufundi wa umeme, kuchomelea mageti.

Katika mwaka wa fedha 2020/2021, halmashauri ya jiji la imetenga kiasi cha shs. 1,225,305,864 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi ambapo katika robo ya kwanza Julai hadi Septemba, Halmashauri imetoa mikopo yenye jumla ya sh228,500,000, huku vikundi 29 vya wanawake kiasi cha sh 167,000,000, vikundi 7 vya Vijana sh 48,000,000 na Vikundi 2 vya watu wenye ulemavu sh13,500,000, huku ikiendelea na mchakato wa kukamilisha utoaji wa mikopo kwa robo ya pili Oktoba hadi Desemba 2020/2021 kiasi cha sh 300,000,000 ambayo ilitolewa mwishoni mwa mwezi Januari 2021.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • UMITASHUMTA & UMISSETA 2025 KUFANYIKA KITAIFA MKOANI IRINGA.

    May 31, 2025
  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.