Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mhe. Mchengerwa aweka jiwe la msingi jengo la jiji Arusha, ashuhudia utiaji saini mikataba ya miradi ya bilioni 40

Imewekwa tar.: May 2nd, 2025

Na John Mapepele 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo  ameweka jiwe la msingi  kwenye jengo la utawala la jiji la Arusha na kushuhudia utiaji wa saini mikataba ya mradi wa Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha, Soko la Mrombo na Bustani ya Mapumziko ya Themi vyote vikiwa na thamani ya takriban shilingi bilioni 40.

Akikagua ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya jiji la Arusha lenye sakafu tisa ambalo litakapokamilika  litagharimu bilioni 9.8 amemtaka  mkandarasi kukamilisha ujenzi kwa wakati ili kuondokana na adha ya sasa ya watumishi kufanyia kazi  kutokea kwenye ofisi zilizo katika maeneo tofauti hali inayochelewesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuridhia kutoa fedha za ujenzi  wa jengo hili kwa kuwa baada ya kukamilika litakuwa mkombozi kwa watumishi" . Amefafanua Mhe. Mchengerwa 

Aidha ameuelekeza uongozi wa Mkoa na Jiji la Arusha kuhakikisha jengo hilo linakamilika mara moja na endapo kutakuwa na mkwamo wowote wachukue hatua.

Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa kukwamua mgogoro wa kushindwa kukamilika kwa jengo hilo kwa zaidi ya miaka 5 kutokana na masuala  ya kisiasa.

Mradi huo  umefikia asilimia 62 na unafanywa na mkandarasi mzawa M/S  Tribe Construction Ltd na unatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu.

Akihutubia wananchi baada ya  kushuhudia utiaji wa saini mikataba ya mradi wa ujenzi wa Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha na Soko la Mrombo na Bustani ya Mapumziko ya Themi, Mhe. Mchengerwa amewataka  viongozi kufanya maaamuzi magumu katika kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Miradi hiyo ambayo inatarajia kugharimu  bilioni 30.6 itakapokamilika ametaka iwe inaweza kujiendesha yenyewe na kutoa faida.

Pia amesisitiza kuilinda, na kufanya usafi ili iwezekudumu kwa muda mrefu pindi itakapokamilika.

"Jukumu letu ni kuitunza miundombinu hii itakayojengwa kwa gharama kubwa ili iweze kudumu kwa muda uliotarajiwa. Aidha, naelekeza Halmashauri zenye Miradi yenye kujiendesha kama Masoko na Stendi zihakikishe miradi hiyo inajiendesha na kuzalisha mapato kwenye Halmashauri husika." Amesisitiza Mhe. Waziri 

Amemtaka mkandarasi  kufanya kazi kwa haraka na kukamillisha kulingana na mkataba na mpango kazi uliokubalika ili wananchi wa Jiji la Arusha waanze kunufaika na miundombinu hiyo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza katika jijini Arusha.

Aidha, amemtaka mkandarasi mshauri kuhakikisha mikataba hiyo inasimamiwa kikamilifu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi na TARURA ili ikamilike ndani ya muda uliopangwa, lakini pia katika ubora uliokubalika ili thamani ya fedha ionekane.

Pia  amewaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri wasimamie kikamilifu utekelezaji wa miradi hiyo kwa kutumia rasilimali watu na vifaa vilivyopo kwenye Halmashauri husika.

Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya Wananchi. Mojawapo ya hatua zinazochukuliwa ni kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, Masoko, pamoja utunzaji wa Mazingira katika maeneo ya mijini chini ya Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Miji ya Tanzania kwa kuhusisha Ushindani ambao kitaalam unajulikana kama Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness (TACTIC) Project.

"Ndugu Wananchi, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatekeleza kwa vitendo falsafa ya maendeleo jumuishi. Miradi tunayoizindua leo kupitia Mradi wa TACTIC siyo miundombinu pekee  bali ni daraja kati ya leo na kesho bora zaidi kwa wananchi wetu." Amesisitiza 

Amesema miradi hiyo inatekelezwa kupitia Mkopo wa Benki ya Dunia utakaogharimu kiasi cha Dola za Kimarekami Milioni 410 na inatekelezwa katika miji 45 mbalimbali nchini. Lengo kuu la mradi wa TACTIC ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa Miji pamoja na kuziwezesha Halmashauri za Miji na Majiji kutoa huduma bora kwa wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.