• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Meatu watakiwa kukamilisha ujenzi wa wodi za akina mama na watoto

Imewekwa tar.: March 6th, 2019

Na Mathew Kwembe, Simiyu

Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu umepewa hadi tarehe 30 machi, 2019 uhakikishe kuwa  unakamilisha ujenzi wa majengo ya wodi ya akina mama na watoto ili huduma  za matibabu katika zahanati na vituo vya afya wilayani humo ziweze kuanza mara moja.

Wito huo umetolewa jana na Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani (UNFPA)  kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dinah Atinda wakati alipoongoza timu ya ufuatiliaji kwenye miradi ya ujenzi wa majengo ya wodi ya akina mama na watoto katika halmashauri hiyo.

Katika ziara hiyo, timu ya ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ilibaini kuwa majengo yote ya akina mama na watoto katika zahanati za Bulyashi, Mwabulutago, Sakasaka, Kisesa, na Itinje hayajaanza kutoa huduma kwa akina mama ya kujifungulia kwa vile hayajakamilika.

Kufuatia hali hiyo Mratibu huyo wa UNFPA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI alieleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ihakikishe kuwa inayakamilisha majengo hayo ili akina mama na watoto waweze kuyatumia kwa ajili ya kupata matibabu.

Bi Atinda aliyataja baadhi ya mapungufu ya majengo hayo kuwa ni pamoja na baadhi yake kutokamilika sehemu ya vyoo, kutowekewa madirisha,  na baadhi yake kuwa na milango mibovu na haina vitasa.

Mbali na changamoto hizo, Bi Atinda aliongeza kuwa baadhi ya zahanati zilikuwa zinakabiliwa na tatizo la kukosa maji ya uhakika na pia baadhi ya majengo vifaa vilivyotolewa na wafadhili UNFPA vilikuwa havijawekwa ndani ya majengo hayo.

Baada ya kuona changamoto hizo, Mratibu wa UNFPA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Atinda aliagiza halmashauri ya wilaya ya Meatu ihakikishe kuwa majengo hayo yanakamilika kabla ya tarehe 30 mwezi huu.

“Hakikisheni majengo haya yanakamilika kwa wakati, fanyeni kila muwezalo fedha itoke mkoani au katika halmashauri ili majengo haya yakamilike,” alifafanua bi Atinda.

Kwa upande wake Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Alex Lyimo alieleza kuwa kila zahanati katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ilipewa shilingi milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha jengo la akina mama na watoto kwa zahanati na shilingi milioni 450 kwa kila kituo cha afya katika wilaya zote za mkoa wa Simiyu.

Katika mchanguo wa fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 250 zilitolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani (UNFPA) na shilingi milioni 200 zilitolewa na Serikali chini ya ufadhili wa nchi ya Denmark

 Bwana Lyimo aliongeza kuwa halmashauri zote zilitakiwa kujenga majengo hayo kupitia mfumo wa ‘force account’ na hivyo kuhakikisha kuwa majengo hayo yanajengwa kwa ubora uliokusudiwa na bila kusababisha upotevu wa fedha.

Naye Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meatu bwana John Kunguku aliyapokea maagizo hayo na kuongeza kuwa  changamoto hiyo imetokana na tathmini ya Mhandisi wa ujenzi wa wilaya kuonyesha kuwa majengo hayo yangejengwa kwa kiasi hicho na kukamilika bila tatizo lolote.

Jumla ya vituo vya afya na zahanati 38 zilipewa fedha katika mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuboresha huduma za akina mama na watoto, fedha ambazo zilitolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani (UNFPA) kupitia shirika la misaada la Korea (KOICA) na pia ufadhili wa Serikali ya Denmark.

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • WAZIRI KAIRUKI AMEKUTANA NA WABUNGE WA MAJIMBO YA MKOA WA TABORA

    February 06, 2023
  • ELIMU YA HUDUMA YA AFYA KUENDELEA KUTOLEWA MASHULENI: DKT. DUGANGE

    February 06, 2023
  • HOSPITALI MPYA ZA WILAYA 135 ZAJENGWA NA RAIS DKT. SAMIA NCHI NZIMA

    February 05, 2023
  • VITUO VYA AFYA SITA VYAJENGWA WANGING’OMBE NDANI YA MIAKA MIWILI YA RAIS DKT.SAMIA

    February 04, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.