Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

MCHENGERWA ATOA MWEZI MMOJA KWA DED MULEBA KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI

Imewekwa tar.: December 15th, 2023

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Dk.Peter Nyanja kukamilisha majengo ya hospitali ya Wilaya.

Pia ametoa siku nne kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Elias Kayandabila (ambaye sasa ni DED Tabora Manispaa) na mhandisi Zefania Chacha kutoa maelezo ya kwanini fedha zilizotengwa Sh. milioni 500 zimeshindwa kukamilisha kazi hiyo.

Ofisi ya Rais-TAMISEMI iilitoa Sh milioni 500 kwa kila Halmashauri isiyo na hospitali ya Wilaya kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa nje na maabara.

Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo  baada ya kutemebelea hospitali hiyo na kuutaka uongozi wa Halmashauri hiyo kutumia mapato ya ndani kukamilisha ujenzi wa magonjwa ya wagonjwa wa nje na maabara ili wananchi aanze kupata huduma wakati majengo mengine ya namalizia.

Alisema kwa kutumia mapato ya ndani Mkurugenzi ahakikishe anamaliza ujenzi wa majengo hayo na kuwa ifikapo Januari,2024 atakuja kukagua ili wananchi wapate waanze kupata huduma.

"Mnakwenda kufanya mapitio ya Bajeti zenu, hakikisheni mnatenga fedha kwa ajili ya majengo haya ili nikija Januari iwe limekamilika kinyume chake nitakusimamisha na kupeleka jina lako kwa Mheshimiwa Rais ili akutengue.

" Kwa walioshindwa kumalizia majengo, Mhe. Mchengerwa alisema inashangaza kuwa serikali inatoka fedha kwa ajili ya miradi lakini baadhi ya Watumishi wanazitumia ndiyo sivyo na kusisitiza kuwa hata kama Mkurugenzi amehama kituo cha kazi lazima atoe maelezo na yafike Ofisini kwake Jumatano ijayo.

"Haiwezekani Rais Samia awaletee wananchi wake fedha za kuwajengea hospitali lakini wengine wanazitumia vibaya hiyo Haiwezekani na wala sitakubali hali kama hiyo."

Alisema fedha ambazo Waziri Mkuu aliahidi ya Shilingi bilioni 1 Serikali itazileta Januari mwakani na kuwa fedha hizo itatumika kujenga majengo mengine ya hospitali.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatuma Mwassa alisema changamoto iliyokuwepo ni usimamizi dhaifu wa miradi na kuwa ameelekeza kutumia mapato ya ndani kukamilisha majengo hayo.

" Halmashauri zingine ambazo ziko mbali zaidi ya hii na maeneo yao yalikuwa mabaya wamekamilisha na majengo yao ni mazuri, shida iko hapa Muleba na Bukoba."

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dk. Abel Mwendawile alisema tayari walishaielekeza TAKUKURU kupitia gharama za ujenzi wa hospitali hiyo.

Naye Dk.Nyanja alisema ili kukamilisha majengo hayo kiasi cha Sh milioni 191.9 zinahitajika na kuahidi kuzitafuta wakati wa kufanya mapitio ya Bajeti ya mwaka 2023/24.

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.