Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mbulu anzeni kupima viwanja, Dongobesh Inakua kwa kasi

Imewekwa tar.: September 13th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuanza kupanga Mji wa Dongobeshi kwa kuwa makao makuu ya Wilaya hiyo yanahamia hapo ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa wa Manyara na kutembelea  ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Mbulu  linalojengwa katika eneo la Dongobeshi.

“Hapa pameshakua mjini sasa maana Jengo la Halmashauri la Gorofa kama hili linaendelea kujengwa na wote watumishi wote mtahamia hapa, bado kuna kituo cha Afya ambacho kimeshakamilika na kuanza kutoa huduma na Serikali inaendelea na Ujenzi wa Hospital ya Wilaya katika eneo hili miradi hii yote kwa kiasi kikubwa itachangia ukuaji na uhamiaji wa watu hivyo ni vyema mkajipanga kuona namna bora ya kupanga mji wenu” Alisema Jafo

Aliongeza kuwa Mnatakiwa muanze kufikiria maeneo yatakayofaa kwa ajili ya upimaji wa viwanja hapa hapatakiwa kuanza kukua kiholela pimeni viwanja  watu wakae kwenye maeneo yaliyopangika na mji uweze kukua vizuri.

Wakati huo huo Waziri Jafo ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa usimamizi makini wa ujenzi wa Jengo la Halmashauri linaloendelea kujengwa katika eneo la Dongobesh.

“Tumewaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala  lakini kukawa na mivutano ya wapi  pangefaa kuwa Makao Makuu ya Wilayah ii ambapo ndipo Jengo hili lilitakiwa kujengwa: Ninachofurahi kuona leo ni kuwa mlipokea maelekezo na jengo limejengwa katika eneo la Dongobesh ambapo ni katikati ya Wilayah ii na rahisi kwa wananchi kufika  kutoka kila pande za Wilaya hii”Alisema Jafo.

Kwa kujenga jengo hili Dongobesh mmewatendea haki Wananchi wa Mbulu kwa kuwa mmewapunguzia gharama ya muda na umbali ambao kwa muda mrefu imewagharimu kufuata huduma za Muhimu katika Ofisi za Serikali aliongeza Jafo.

“Nimeridhishwa  na ujenzi unaoendelea na nimefurahi kuona mmeshakamilisha majengo ya chini, nimeridhishwa na ubora wa Jengo pamoja na  gharama  nafuu toka kwa Mkandarasi Mzinga holding Company pamoja na Mhandisi Mshauri Dar es salaam Institute of Technology (DIT) niseme kazi nzuri na hongerni sana ” alimalizia Jafo.

Akiwasilisha ripoti ya ujenzi wa Jengo la Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Hudson Kamoga amesema ujenzi  wa jengo la Utawala unafanyika kwa awamu tatu na katika awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa jengo la mbele ambalo litagharimu tsh Bil 4.7  awamu ya pili itahusisha ujenzi wa ukumbi, ghala na mgahawa na awamu ya tatu utahusisha ujenzi wa pande mbili za nyuma ya jengo.

Kamoga aliongeza kuwa Jengo hilo la Utawala limekadiriwa kujengwa kwa gharama ya Tsh 6.7 ambapo gharama za ujenzi ni Bil 6.3 na gharama sa mhandisi mshauri ni mil 351 huku gharama sa kuandaa mchoro zikigharimu tsh mil 30 tu.

Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Mbulu umetokana na kugawanyika kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kupatikana kwa  Halmashauri ya Mji wa Mbulu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu  na kupelekea Mbulu Mji kubakia Mjini na Halmashauri ya Wilaya kuhamia katika eneo la Dongobesh ambapo ujenzi huo unaendelea.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.