Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Mapinduzi Makubwa Bajeti za Halmashauri 2018/2019

Imewekwa tar.: March 2nd, 2018
Timu ya wataalam 50 kutoka Makao Makuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri imefanikiwa kukamilisha uchambuzi wa bajeti za Halmashauri 185 za Tanzania Bara kwa njia ya Kielektroniki kwa mwaka wa fedha 2018/2019 . Bajeti hiyo inakadiriwa kufikia wastani wa Shilingi trilioni 6.

Akielezea mara baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa bajeti, Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ndugu Beatrice Kimoleta alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Mamlaka ya serikali za Mitaa kufanya Bajeti kwa njia ya Kieletroniki ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu.

“Itakumbukwa kuwa wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu akizindua Mfumo wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (PlanRep) mwezi Septemba, 2017 aliagiza kwamba bajeti zote za Halmashauri za mwaka wa fedha 2018/2019 zitumie mfumo mpya wa PlanRep iliyoboreshwa. Hivyo, huu ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.” Amenukuliwa Kimoleta.

Mmoja ya Wakufunzi wa timu ya uchambuzi wa bajeti, Allan Bendera ambaye ni Mchumi kutoka idara ya Mipango na Sera Wizara ya TAMISEMI alisema kwamba mfumo huo mpya umesaidia kupunguza gharama za fedha ambazo zilikuwa zikitumika wakati wa uchambuzi wa bajeti.

“Gharama ni moja ya jambo ambalo limepunguzwa sana kupitia uchambuzi wa bajeti kwa njia ya kielektroniki kama ilivyokusudiwa hapo awali. Lakini pia, mfumo umeokoa muda mwingi uliokuwa ukitumika wakati wa mapitio ya bajeti kwa kiasi kikubwa.” amesema Bendera.

Bajeti hiyo ambayo kwa mujibu wa Mchumi Willison Gwoma, kutoka Wizara ya TAMISEMI  inakadiriwa kufikia kiasi cha Shilingi trilioni 6 na imewashirikisha wanachi kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.

Akitoa salaam kwa timu iliyokamilisha uchambuzi wa bajeti Ndugu Samson Hango, kutoka Idara ya Elimu Wizara ya TAMISEMI aliomba baadhi ya changamoto zilizojitokeza hususan katika sekta ya elimu zifanyiwe maboresho.

“Tunaomba katika mwaka ujao wa maandalizi ya bajeti, Wataalam walioandaa mfumo waboreshe Majedwali ya takwimu za kielimu ili kurahisisha uingizaji wa bajeti za sekta hiyo” amesema Hango.

Suala la maandalizi ya mipango na bajeti kwa njia ya kielektroniki ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb)  wakati akizindua mfumo wa PlanRep iliyo boreshwa 5 Septemba, 2017 ili kuondokana na matumizi makubwa ya rasilimali muda, fedha pamoja na shajala ambazo zilikadiriwa kufikia wastani wa Shilingi bilioni 4

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.