Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri waaswa kusimamia Programu za Elimu ya Watu Wazima

Imewekwa tar.: October 10th, 2024

Na Fred Kibano, Tabora

Serikali imewataka Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kusimamia Programu za Elimu ya Watu Wazima ili kuongeza maarifa, ujuzi na stadi zitakazowasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo tarehe 10 Oktoba, 2024 Manispaa ya Tabora katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyn Nombo wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ambapo ametoa wito kwa Viongozi hao kusimamia Programu za Elimu ya Watu Wazima ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

“ninaomba Viongozi na Wadau kushiriki kikamilifu katika programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ili kupata maarifa, ujuzi na stadi mbalimbali kwa lengo la kujiletea maendeleo, nawaomba Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi zinazotekelezwa katika maeneo yenu” alisema Prof. Carolyn Nombo.

Amezitaja baadhi ya Programu hizo kuwa ni pamoja na Mpango wa Uwiano wa Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA), Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana (MECHAVI au IPOSA), Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) na Vituo vya Wazi vya Ujifunzaji (Open Learning Centres) kwa elimu ya sekondari.

Aidha, Prof. Nombo amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 inasisitiza unyumbufu wa elimu na elimu bila ukomo inayozingatia matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika juhudi za maendeleo binafsi, jamii na Taifa kwa ujumla hivyo ni vema Viongozi wote kuisimamia.

Kwa upande wake Mwl. Ernest Hinju Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Watu Wazima, Elimu Maalum, Elimu nje ya Mfumo Rasmi na Michezo alisema katika miaka mitatu sasa Elimu ya Watu Wazima inafanya vizuri nchini kwani idadi ya wanaofanya mitihani na kufaulu imeongezeka kama MEMKWA lakini pia inasaidia kuleta maendeleo ya jamii hususani katika uchumi, ushirika na kilimo.

Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Maafisa Elimu Watu Wazima Mkoa wa Iringa Martha Luambano amesema kikao kazi cha siku mbili chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na kongamano chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia vitawasaidia kufanya tathmini ya majukumu yao na wataweza kuendesha Programu za Elimu ya Watu Wazima kwa ufanisi kwenye maeneo yao pamoja na kuisambaza kwa jamii.

Maadhimisho ya juma la Elimu ya Watu Wazima hapa nchini huadhimishwa kila mwaka katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya kwa kushirikisha Wadau na Taasisi mbalimbali zinazotekeleza programu za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ili kubaini changamoto na namna ya kukabiliana nazo. Kaulimbiu ya mwaka 2024 ni “Ujumuishi katika Elimu bila Ukomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu, Amani na Maendeleo”  

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA VITUO VYA AFYA.

    May 19, 2025
  • MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI WAPEWA SOMO USIMAMIZI WA MIRADI NA USULUHISHI WA AKAUNTI

    May 19, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.