Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Makatibu Tawala Mkoa na Wakurugenzi kuwasilisha taarifa za miradi kwa wakati.

Imewekwa tar.: March 10th, 2019

Makatibu Tawala wa Mikoa  na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wote nchini wametakiwa kuhakikisha kila idara   inawasilisha  taarifa sahihi na kwa wakati  ili, kuweza kuimarisha tathmini ya kasi ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali na kubaini mafanikio na changamoto na kuchukua hatua stahiki kwa wakati.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt. Dorothy Gwajima kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma.

Amesema kuwa, upatikanaji wa taarifa kuanzia ngazi ya Halmashauri, Mikoa bado ni changamoto kubwa hali ambayo inasababisha kurudisha nyuma kasi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

“Taarifa ya mpango wa malipo kwa ufanisi (RBF) umechukua miezi 3 na cha kushangaza, mara baada ya kutoa notisi ya saa 72 kuwa, Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakabidhi majukumu ya uongozi iwapo watashindwa kuwasilisha na warudi kwenye kazi zao za kitaaluma, wote waliwasilisha kabla hata ya muda huo, kitu kinachodhihirisha kuwa, kuna uzembe katika uwajibikaji. Hivyo, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri hakikisheni mnawasimamia wataalamu walio chini yenu kuwajibika kikamilifu na kwa wakati” Amesema Dkt. Gwajima

Akiongelea kuhusu utoaji wa taarifa za ujenzi wa Hospitali za mpya  (67) za Halmashauri za Wilaya amesema kuwa, Waganga Wakuu wa Mikoa waliagizwa kuwasilisha taarifa hizo wiki mbili zilizopita lakini, mpaka sasa ni mikoa sita tu ndiyo imetoa taarifa.

Aidha, mikoa mingine iliyowasilisha, taarifa hizo hazijakamilika hivyo, amewaagiza Waganga Wakuu Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha wanawajibika kuwasaidia kikamilifu viongozi wao. Alisema “kuwe na mpango wa ujenzi wa vituo unaoonesha nini kinafanyika kila wiki na taarifa ya utekelezaji iwasilishwe kila wiki Wizarani”

Aidha, Dkt. Gwajima amesema kuwa, kila Katibu Tawala wa Mkoa husika na Mkurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ahakikishe  vituo vya afya vyote  vilivyokamilika vinawezeshwa kuanza kutoa huduma kwa kutumia raslimali za ndani ya halmashauri badala ya kusubiri kila kitu toka Serikali kuu.

 Amesema, inawezekana kuanza kutoa baadhi ya huduma kwa kutumia rasilimali toka halmashauri husika kama ilivyofanyika kwenye halmashauri zingine. Aidha, wale wanaoendelea na ujenzi au ukarabati wasimamie wakamilishe.

Dkt. Gwajima ameendelea kusema kuwa kila Halmashauri ihakikishe inatumia mifumo ya kielektoniki katika ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vyote vya afya ili kuepusha mianya ya upotevu wa fedha za Serikali.

Amesema  kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya watoa huduma kutafuta visingizio vya kutotumia mifumo hii hivyo wajue kuwa, matumizi ya mifumo hii ni lazima na haikwepeki”

Kuhusu fedha zilizotengwa kwa ajili ya kazi za maendeleo Dkt. Gwajima amesema, zitumike kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo na kinyume na hapo, hatua kali zitachukuliwa.

Dkt. Gwajima amewataka Makatibu Tawala na Wakurugenzi kuwasimamia wataalamu wa afya kuwa wabunifu katika  kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za afya kwa kuimarisha utoaji wa huduma za tiba kwa mkoba kwa kualika wataalamu ambao, wanakosekana katika maeneo husika ili, kuongeza kasi ya kusogeza huduma kwa wananchi na kuwapunguzia adha ya kusafiri mbali kufuata huduma hizo.

 “Unaposogeza huduma za Afya karibu na wananchi kwa njia ya mkoba, hata uwezo wa wananchi kuchangia unakuwa mkubwa maana, unawapunguzia gharama ya nauli na gharama za maisha mbali na makazi yao” Anasema Gwajima.

Aidha Dkt. Gwajima ametoa wito kwa viongozi hao kutochukua  hatua za kinidhamu kwa watumishi bila kufuata taratibu za kiutumishi kwa maana, unapochukua hatua kinyume na taratibu ukumbuke kuwa, hilo ni kosa kwa mujibu wa miongozo na taratibu za utumishi wa umma .



Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.