• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
    • Ramani za mradi wa BOOST
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA SHIRIKIANENI NA WANANCHI KUTATUA KERO ZAO

Imewekwa tar.: June 6th, 2023

Asila Twaha, Songwe

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Sospeter Mtwale amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata  kutoa elimu kwa wananchi na kushirikiana kutatua kero zao. 

Mtwale ameyasema hayo Mei 05, 2023 alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya   kuwajengea uwezo viongozi wa Halmashauri, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata wa Mkoa wa Songwe lengo ni kuongeza uwezo na ufanisi kutekeleza majukumu yao.    

“mafunzo haya sio tu kwa Mkoa wa Songwe bali yatafanyika nchi nzima ili kuwaongezea uwezo wa kutekeleza majukumu yenu na kuwa karibu na wananchi sababu mambo mengi yanaanzia kwenu” Mtwale

Amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watumishi na ilishatoa vitendea kazi kama pikipiki kwa Maafisa Tarafa  kwa ajili kurahisisha shughuli  za kiutendaji hasa  kusikiliza kero na changamoto za wananchi.

“msisubiri mpaka viongozi wakubwa wafike kwa wananchi ndio watatue kero kafuatilieni na kuhimiza utekelezaji wa Sera za Serikali kila mtu katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo kwa kutenda haki na kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu”

Mtwale amesema, uzoefu unaonesha kuwepo kwa changamoto zinazoathiri utoaji wa huduma kwa wananchi katika ngazi ya Kata,Tarafa na Halmashauri zinazotokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji kazi wa kila siku.

Amefafanua changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa migogoro ya kiutendaji kati ya wataalam  na viongozi na wataalam wengine katika ngazi hizo, ufuatiliaji na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye ngazi za msingi, kutotatuliwa kwa wakati kero za wananchi na wadau wengine katika ngazi za msingi na kutokuwa na uelewa katika baadhi ya Sera, Sheria na Miongozo inayotakiwa kusimamiwa na kuitekeleza.

Amesema Mtendaji Mkuu wa Kata  ni kiungo cha uongozi kwa Idara zote kwenye Kata  hivyo, anatakiwa kushiriki, kutoa ushauri kuhusu upangaji wa mipango ya maendeleo katika eneo lake lakini pia kusimamia upangaji wa Mipango Shirikishi ya Maendeleo ya Kata na kupokea na kutatua matatizo na malalamiko ya wananchi katika kata.

Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda ameshukuru uongozi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kuandaa mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata amesema wataalam hao ndio watendaji wa moja kwa moja kwa wananchi.

Naye Afisa Tarafa Kamsamba Halmashauri ya Wilaya ya Momba Bw. Haji Ibrahim ameishukuru Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kuandaa mfunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo amesema kama mtumishi wa umma akijengewa uwezo inasaidia kufanya kazi zake kwa ufanisi lakini matarajio yaliyokusudiwa na Serikali kuyatimiza.

Aidha amesema, kunautofauti ya mtu aliyejengewa uwezo katika mafunzo na asiyejengewa uwezo, katika mafunzo hayo kupitia mada tutakazofundishwa itatusaidia kuongeza ufanisi katika majukumu  yetu na kubadilika kwa kutumia mbinu tulizofundishwa kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi katika kazi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTWA KAZINI September 13, 2023
  • Terms of Reference TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS PROJECT (TACTIC) September 01, 2023
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI,2023 September 22, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA MPYA 2023 AWAMU YA PILI August 30, 2023
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO KWA SHULE MPYA ZA SEKONDARI,2023 August 25, 2023
  • KUSIMAMISHWA KAZI KWA MKURUGENZI WA BUHIGWE July 12, 2023
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • NDEJEMBI ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATAALAM WA ELIMU

    September 18, 2023
  • DKT. SAMIA ASHANGAZWA NA HALMASHAURI KUSHINDWA KUJENGA JENGO LA X-RAY

    September 17, 2023
  • SHULE ZA MSINGI 1,000 KUJENGWA NCHI NZIMA

    September 17, 2023
  • TRILIONI 6.5 ZATEKELEZA MIRADI YA ELIMU, AFYA NA MIUNDOMBINU

    September 15, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.