Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata watakiwa kufuatilia na kusimamia miradi

Imewekwa tar.: August 5th, 2024

Na Fred Kibano, Manyara 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kusimamia miradi ya maendeleo ili kuondoa changamoto za kutokukamilika kwa miradi hiyo.

Mheshimiwa Sendiga ameyasema hayo mapema leo tarehe 05 Agosti, 2024 mjini Babati wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata ambapo amebainisha kuwepo kwa changamoto zinazosababisha kutokamilika kwa miradi kutokana na usimamizi na ufuatiliaji hafifu.

“tunakutana na changamoto nyingi za ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo ambayo hairidhishi katika maeneo mengi, tukikuta mradi una changamoto kwenye eneo lako basi Mtendaji wa Kata hapo umepwaya” alisema Mheshimiwa Queen Sendiga.

Aidha, Sendiga amesema uwepo kwa changamoto hizo unaathiri utoaji wa huduma kwa wananchi katika ngazi ya Kata na Tarafa zinazotokana na kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji kazi wa kila siku wa watendaji hao kama vile kuwepo kwa migogoro ya kiutendaji kati ya Wataalam hao na viongozi na Wataalam wengine katika ngazi hizo.

Changamoto nyingine ni pamoja na kutotatuliwa kwa wakati kero za wananchi na wadau wengine katika ngazi za msingi jambo linalosababisha wananchi kwenda kupata suluhu ngazi za juu ofisi ya Mkoa au Wilaya kwani zaidi ya asilimia 90 ya kero zinatokana na migogoro, kesi, malalamiko, ambazo Maafisa hao wanaweza kuzifanyia kazi na kushindwa kwao nao wanakuwa sehemu ya kero inayotakiwa kufanyiwa kazi.

Mhe. Sendiga amesema Afisa Tarafa ndiye Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa na Mtendaji wa Kata ni kiungo cha Uongozi kwa Idara zote kwenye Kata na hivyo Serikali inawategemea wao kama kiungo muhimu katika ngazi ya msingi.

Naye Bi. Beatrice Kimoleta Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na ofisi yake kupitia Programu ya Uimarishaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Regions and Local Government Strengthening Programme-RLGSP)

Aidha, amesema mafunzo haya yametolewa kwa awamu katika Mikoa 18 ya Tanzania Bara na hadi sasa mafunzo hayo yametolewa kwa washiriki 3,094 ambapo kati ya hao Maafisa Tarafa ni 340 na watendaji wa Kata 2,754 na katika awamu hii ya mwisho inahusisha mikoa nane ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma ambapo Maafisa Tarafa 203 na Watendaji wa Kata 1,377 watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo.

Kwa upande wake Msala H. Msala Afisa Tarafa ya Babati amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuleta mafunzo hayo kwani yatamjengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku lakini pia kuboresha huduma kwa wananchi kupitia elimu kama vile kufanyika kwa mikutano ya kijamii.




Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.