Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Maafisa Elimu waaswa kuleta mageuzi ya Elimu ya Watu Wazima nchini

Imewekwa tar.: October 8th, 2024

Na Fred Kibano, Tabora 

 Mkurugenzi Msaidizi, Elimu ya Watu Wazima, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mwalimu Ernest Hinju   amewataka Maafisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri nchini kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuleta mageuzi kwenye Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

Mwalimu Ernest Hinju ametoa wito huo leo tarehe 08, Oktoba 2024 wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Maafisa Elimu Watu Wazima chenye lengo la kutathmini utendaji kazi wao, kilichofanyika Manispaa ya Tabora katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Mwalimu Ernest Hinju amewataka Watendaji hao kutumia fursa ya kikao kazi hicho kufanya tathmini ya utendaji kazi wao nchini ili kuleta mapinduzi makubwa kwenye Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.

“Kikao hiki kitumike kufanya tathmini ili kuona kwa kiasi gani tunatekeleza kwa ufanisi shughuli zote za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi na hatimaye mje na mikakati ya kuboresha utendaji kazi,” Mwalimu Ernest Hinju amesisitiza.

Mwalimu Hinju amesema kikao hicho pia kinapitia maazimio ya kikao kama hicho kilichofanyika mkoani Morogoro mwaka 2024 kikitoa fursa ya kupeana ujuzi, uzoefu, kutambua nafasi zao, kujua changamoto za Elimu ya Watu wazima pamoja na kudumisha umoja, ushirikiano na upendo miongoni mwa Maafisa hao ili kuboresha utendaji wao kwa manufaa ya watanzania. Aidha, kikao hicho kilitoka na maazimio ambayo pia utekelezaji wake utawasilishwa katika kikao kazi hiki.

Akiongea kwa niaba ya Afisa Elimu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aron Vedasto amezishukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa kikao kazi hicho kama sehemu ya maadhimisho ya juma la Elimu ya Watu Wazima mkoani Tabora kwani wataweza kujitathmini kama mkoa. lakini ameahidi kuhakikisha wanainua Elimu ya Watu Wazima  

Sanjari na hilo, Bw. Aron Vedasto ameahidi kuwa, watahakikisha wanainua Elimu ya Watu Wazima kwani kwa mujibu wa takwimu za sensa mwaka 2022 zinaonyesha mkoa huo ndio unaoongoza kuwa na idadi kubwa ya watu wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa miongo miwili mfululizo.

Naye Bw. Florence Njiku Afisa Elimu Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Mara, akiwasilisha taarifa ya mkoa amesema mkoa wake una jumla ya wanakisomo wa MUKEJA 1357, MEMKWA 2463, wasichana waliokatishwa masomo kupitia SEQUIP 179 huku walimu na watu mbalimbali wakitumia Programu ya Elimu Masafa na Elimu ya ana kwa ana (ODL), hivyo wamefanikiwa kuwa na jamii yenye mwamko wa kuwarejesha masomoni wanafunzi wengi walioacha shule na wale waliokatishwa masomo.

Kikao kazi hicho cha siku mbili ni sehemu ya maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima Kitaifa yanayofanyika mkoani Tabora ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikihusisha baadhi ya Taasisi za Wizara hizo na Wadau mbalimbali huku kukiwa na kongamano na maonyesho.  Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Ujumuishi katika Elimu bila ukomo kwa ujuzi, ustahimilivu, amani na maendeleo”

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali kutumilia Bilioni 208.9 kuwezesha kaya duni laki mbili na elfu 60 kwa miaka sita

    May 15, 2025
  • Naibu Katibu Mkuu Mwambene aendesha kikao kazi kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya

    May 14, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUTOA  MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE.

    May 13, 2025
  • HALMASHAURI ZATAKIWA KUSIMAMIA ZOEZI LA USAFI WA BARABARA

    May 13, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.