Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Ma DC na Ma DED Wapya Waaswa Kutatua Kero za Wananchi

Imewekwa tar.: October 12th, 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kutatua kero za wananchi na kusimamia vema rasilimali za Serikali ili kuendana na dhamira ya Rais John Pombe Magufuli.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya Wakurugenzi wapya wa Halmashauri na Wakuu wapya wa Wilaya yaliyokuwa yakifanyika Jijini Dodoma mapema wiki hii.

Waziri Jafo amewaagiza viongozi hao kutatua kero za wananchi kwa wakati na kuwa na ajenda ya Kudumu ya kuhakikisha wanatengeneza fursa za kiuchumi na ajira ili kuwainua kiuchumi vijana, akina mama na walemavu waliopo katika wilaya zao, lakini pia kuzingatia usafi na kuhakikisha wanapambana na Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya ambazo zinaathiri sana nguvu kazi ya vijana na hivyo waweke mikakati ya kuzuia na jinsi ya kupambana na janga hili.

Kuhusu rasilimali amewaagiza kwenda kubaini rasilimali mpya ambazo wengine walikuwa hawajaziona na kukakikisha zile zilizopo zinakuwa katika hali na matumizi mazuri na kuendelea kuwa hivyo kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa kuzisimamia na kuhakikisha hazitumiki vibaya. “Tumieni sheria, taratibu kanuni na bila kumnyanyasa yeyote kasimamieni rasilimali” alisema Jafo.

Aidha, Waziri Jafo amewaasa Viongozi hao kuzingatia mipaka ya kazi zao, nidhamu,kuepuka kufanya kazi kwa mazoea, kuwa na mahusiano mazuri baina yao na wananchi, kusimamia na kuhakikisha miundo mbinu inakuwa katika ubora unaotakiwa, usafi wa wilaya na halmashauri zao na kusimamia manunuzi mazuri na halali yenye manufaa kwa jamii kuanzia steji ya awali kabisa ya maombi.

Waziri Jafo alisema pia kuwa huduma bora za afya kwa wananchi zimeboreshwa kupitia Serikali ya Awamu ya tano ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania na tayari ameridhia kiasi cha fedha shilingi bilioni 333/= kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya 67 na ifikapo Novemba mwaka huu kila wilaya itapatiwa bilioni 1.5/= kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hizo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe ameowaonya viongozi hao juu ya matumizi mabaya ya madaraka kwani hupelekea wananchi kutafsiri kwamba hayo ndio maelekezo wapewayo.

“Ninawataka kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa na serikali katika nafasi zenu ambazo wananchi wanawaamini, ili mumtendee haki Rais pia.” Alisema Mhandisi Iyombe.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara Mheshimiwa Moses Joseph Machali mmoja kati ya Viongozi hao waliopatiwa mafunzo alitoa tamko la ahadi ya kuzingatia mafunzo hayo na kuishukuru Ofisi ya Rais - TAMISEMI pamoja na Taasisi ya UONGOZI kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi.


Awali akitoa neno la utangulizi Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI Beatrice Kimoleta amesema mafunzo hayo ya siku nne yaliandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Tasisi ya UONGOZI na yalibeba mada tisa ambapo mada kuu ikiwa ni kusimamia Ulinzi, Usalama na Amani katika maeneo yao na hivyo zitawaongoza katika shughuli zao za Kiuongozi na kuleta mahusiano mazuri baina yao na wananchi.


                                  Anaandika Fred Kibano

Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.