• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Kipenga cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa chapulizwa

Imewekwa tar.: August 23rd, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ametangaza rasmi uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya mtaa, kijiji na kitongoji unatarajiwa kufanyika Novemba, 24 mwaka huu.

Akitoa tangazo la uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2019 katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zilizoko katika eneo Mtumba Jijini Dodoma Mhe. Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha wanazingatia miongozo na kanuni za uchaguzi huo.

Mhe. Jafo amesema kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 ibara 4(1-3), Matangazo ya Serikali Na. 371, 372, 373 na 374) ya mwaka 2019, Waziri mwenye dhamana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anautangazia umma wa Watanzania na Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu kuwa tarehe 24 Novemba, 2019 itakuwa ni siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara.

“Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kifungu cha (1) Waziri mwenye thamana na serikali za mitaa anapaswa kutoa Tangazo la Uchaguzi kwa Umma si chini ya siku 90 kabla ya siku ya uchaguzi”. Anafafanua Mhe. Jafo

Mhe. Jafo anaeleza zaidi kuwa tarehe hiyo imepangwa baada ya kukamilika kwa kanuni ambazo zitatumika kuendesha uchaguzi huo ambapo wadau, vyama vya siasa na asasi za kiraia zilishirikishwa na kutoa maoni yao.

“Uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa bora, kwasababu umekuwa shirikishi wakati wa uandaaji kanuni na tumeandaa kanuni ambazo zinaondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza kwenye chaguzi zilizopita” Amesema Mhe. Jafo

 Ameelezea kuhusu siku ya uchaguzi kuwa upigaji wa kura utaanza saa 2:00 asubuhi na kumalizika saa 10:00 jioni na watu watapiga kura kwa karatasi maalum ambazo zitatakiwa kutumbukizwa katika masanduku maalum ya kupigia kura

 Ameendelea kufafanua kuwa kampeni za uchaguzi huo zimepangwa kufanyika kwamuda wa siku saba kabla ya uchaguzi, ambazo zitaanza Novemba 17 hadi 23 mwaka huu.

“ Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kwa muda wa  siku saba kabla ya siku ya Uchaguzi. Ambapo kila Chama cha Siasa kinachoshiriki Uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya kampeni ya Uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni.” Amesema Mhe. Jafo

Ameeleza kuwa nafasi zitakazogombewa ni Mwenyeviti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo, mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji.

Mhe. Jafo ameendelea kuzitaja nyingine kuwa ni nafasi za mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake), Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi la Wanawake) na Wenyeviti wa Vitongoji katika Mamlaka za Wilaya.

Pia Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake), Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi la Wanawake) na Wenyeviti wa Vitongoji katika Mamlaka za Miji.

Kuhusu wagombea Mhe. Jafo amesema wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi watatakiwa kuwa wanachama na kudhamininiwa na Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu.

Mhe.Jafo ameendelea kueleza kuwa  ili kuwafahamisha wananchi majina ya maeneo na mipaka ambayo itahusika katika kujiandikisha na upigaji wa kura, msimamizi wa Uchaguzi atatangaza majina na mipaka ya Vitongoji vilivyoko katika eneo la Halmashauri husika siku 72 kabla ya siku ya uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Mtaa, Wajumbe wa Serikali ya Kijiji na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa.

Amesema msimamizi wa uchaguzi atatoa maelekezo ya Uchaguzi siku sitini na mbili kabla ya siku ya uchaguzi na atafanya uteuzi wa watumishi wa umma watakaoandikisha na kuandaa Orodha ya Wapiga Kura siku 52 kabla ya siku ya Uchaguzi.

“Uandikishaji na uandaaji wa Orodha ya Wapiga Kura utaanza siku ya arobaini na saba (47) kabla ya siku ya uchaguzi na utafanyika kwa muda wa siku saba kwa kutumia fomu maalumu na utafanyika katika majengo ya umma na pale ambapo hakuna jengo la umma, uandikishaji utafanyika kwenye sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atakuwa amekubaliana na Viongozi wa Vyama vya Siasa.

Mhe. Jafo ameendelea kufafanua kuwa vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia kura, kwa maeneo yaliyo chini ya Halmashauri za Wilaya na Mamlaka za Miji Midogo vitakuwa katika ngazi ya Kitongoji na kwa upande wa Mamlaka za Miji (Miji, Manispaa na Majiji), vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia kura vitakuwa katika ngazi ya Mtaa

Amesema kuwa mtu anayekusudia kugombea nafasi za uongozi, atatakiwa kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi husika siku zisizopungua 26 kabla ya siku ya uchaguzi kwa kadri itakavyoelekezwa na Msimamizi wa Uchaguzi.

Hata hivyo, Kuhusu ukomo wa madaraka Mhe Jafo amesema kuwa viongozi wote walioko madarakani kwenye nafasi zote zitakazogombewa, uongozi wao utakoma siku 7 kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombe.

“Nafasi zote zinazogombewa zilikuwa na uongozi kwa kipindi cha miaka 5. Kwa mujibu wa Kanuni hizi, viongozi hao watakoma kushika nafasi za uongozi siku saba kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombea uongozi chini ya Kanuni hizi” Amesema Mhe. Jafo

Amesema mgombea amabye hataridhika na maamuzi ya msimamizi au msimamizi msaidizi wa uchaguzi kuhusu uteuzi atakata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa inayopewa wajibu wa kusikiliza mapingamizi.

“Endapo wagombea hawataridhika na maamuzi ya Msimamizi au Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi kuhusu uteuzi wa wagombea, kutakuwa na Kamati ya Rufaa katika kila Wilaya ambayo itasikiliza mapingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea katika Wilaya husika” Amesisistiza Mhe. Jafo.

Wakati huohuo Mhe. Jafo amesema waangalizi wa ndani wa uchaguzi wanatakiwa kuomba kibali cha kufanya hivyo kwa katibu Mkuu Tamisemi kuanzia Agosti 26 hadi Septemba 16 mwaka huu ikiwa ni ndani ya siku 21 baada ya tangazo la uchaguzi kutolewa.

 Aidha amewaomba wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, kupiga kura, kugombea na kushiriki katika Uchaguzi huu ili kupata viongozi bora wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo ya nchi yetu.

 Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI



Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.