Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

KAMATI YA LAAC YAITAKA HALMASHAURI YA MBULU KUTEKELEZA MAAGIZO ILIYOYATOA

Imewekwa tar.: March 18th, 2024

Na. Asila Twaha, Mbulu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeitaka Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu kufanyia kazi ushauri na maagizo iliyoyatoa mara baada ya kamati hiyo kufanya ukaguzi na kubaini baadhi ya  changamoto katika  utekelezaji wa Mradi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na Shule ya Sekondari Tumati.

LAAC imetoa maelekezo hayo Machi 17, 2024 wakati ilipofanya ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya Mbulu Mkoani Manyara.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Ester Bulaya (Mb) amewahasa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kutekeleza kikamilifu majukumu yao pindi wanapopewa dhamana ya kusimamia fedha za umma katika utekelezaji wa mradi ili ikamilike kwa wakati na ubora pamoja na kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa.

“Hizi fedha za miradi ni za wananchi hivyo ni vema mkawa na uchungu nazo na kuzisimamia ili ziwe na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi,” Mhe. Bulaya amesisitiza.

Awali, ikisomwa taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbulu na ujenzi wa miundombinu ya Kidato cha Tano na cha Sita  ya shule ya sekondari Tumati,  Kamati iliitaka halmashauri hiyo kuondoa changamoto zote zilizobainiwa na kamati katika shule ya sekondari Tumati na kufuata taratibu na miongozo iliyotolewa  na Ofisi ya Rais -TAMISEMI.

Aidha, kamati hiyo iliitaka halmashauri kukamilisha  miundombinu ya maji kwenye vyoo katika shule hiyo ya Sekondari ya Tumati kabla ya kukamilika kwa mwaka huu wa fedha 2023/24.

Kwa upande wa utekelezaji wa mradi wa hospitali, Kamati imemuelekeza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu kuhakikisha fedha walizoingiziwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Kamati imeelekeza fedha  shilingi milioni 500 zilizopokelewa kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu ambazo ni  ya watoto, wanaume na wanawake zitumike kama ilivyopangwa na si kukamilisha miradi viporo.

Sanjari na hilo, LAAC imeitaka Ofisi ya Rais – TAMISEMI kushirikiana na Ofisi ya RAS kufanya tathmini ya kina kuhusu ufanisi wa utekelezaji wa miradi ili hatua stahiki iweze kuchuliwa dhidi ya wataalamu waliohusika kukwamisha utekelezaji wa miradi.

Naye, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Charles Msonde ameihakikishia Kamati  ya LAAC kuwa, TAMISEMI itafuatilia na kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya kamati ili  thamani ya fedha ionekane na wananchi wanufaike na miradi.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.