Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

JAFO: Vijana acheni historia katika utendaji kazi wenu.

Imewekwa tar.: August 15th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo amewataka vijana wanaoteuliwa kufanyakazi kwenye maeneo yoyote nchini kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi ili kuacha alama ambayo haitafutika nchini.

Ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vijana iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Mhe Jafo amesema Vijana wanaopewa nafasi za kuongoza kuacha kufanya kazi kwa maigizo na badala yake wachape kazi katika kuwahudumia wananchi ili kuacha historia katika jamii.

“Vijana acheni maigizo fanyeni kazi ya kuwasaidia Watanzania fanyakazi kwa ajili ya kuwahudumia watu,fanya kazi yako itangazike,tukifanya maigizo hatuwezi kulisaidia Taifa letu” Anasisitiza Mhe. Jafo

Mhe. Jafo anaendelea kufafanua kuwa kila kijana akiwajibika katika nafasi yake aliyopewa atalisaidia taifa kukuwa kiuchumi na hatimaye kufikia uchumi wa kati hivyo nawaagiza vijana kuhakikisha mnatimiza majukumu yenu katika nafasi mnazopewa kwenye jamii.

“Vijana mkipewa nafasi fanyeni kazi, usikubali kuondoka sehemu bila kuacha alama lazima uache alama ili wakukumbuke,kijana kuwa mfano wa kuigwa katika jamii inayokuzunguka,”alisema Jafo.

Mhe. Jafo amewataka vijana kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika sekta zote kwa kubadilisha mitazamo na kuleta maendeleo katika jamii ili nchi iweze kusonga mbele.

Wakati huohuo amewataka kuchangamkia fursa ya mikopo ambayo imekuwa ikitolewa na Halmashauri ambapo amedai kwa sasa kina mama ndio wamekuwa wakichangamkia fursa hiyo.

Amesema Serikali kupitia Halmashauri zote nchini imeweza kutenga fedha za mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu lakini wanaojitokeza hadi sasa kuchukua fedha hizo ni wanawake pekee jambo ambalo si jema katika kuleta maendeleo kwa jamii.

“Inasikitisha kuona Serikali kupitia Halmashauri zake imeweza kutenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu lakini wanaokopa kwa wingi ni kina mama hili si jambo jema kabisa nawahamasisha vijana kukopa fedha ili kujikwamua kiuchumi.” Amesema Jafo

Kwa Upande wake,Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Vijana,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Zanzibar,Amour Hamil Bakari,amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea na juhudi zake za kuhakikisha vijana wanapata kazi pamoja na kufanya kazi zenye staha.

 “Serikali itaendelea kuhakikisha vijana wetu wanapata kazi zenye staha pamoja na changamoto ya ajira.Niwakumbushe vijana kuendelea kulinda amani iliyopo, suala la kudumisha muungano wetu hili halina mjadala na sisi tutaendelea kuwakumbusha vijana kuhakikisha wanalinda muungano kwa nguvu zote,”Amesema Bakari

Naye,Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Jacqueline Mahon alisema vijana  wanatakiwa kusaidiwa katika kutatua changamaoto mbalimbali ili kuwawezesha kuleta mabadiliko katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.