Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Jafo: Natamani kuona Halmashauri zinajitegemea

Imewekwa tar.: December 29th, 2020

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe, Selemani Jafo amesema ndani ya miaka mitatu ijayo matamanio yake ni kuona Halmashauri zinajitegemea zenyewe kupitia mapato ya ndani na kwamba ifike muda ziwe zinalipa watumishi wake mishahara.

Waziri Jafo ameonyesha matamanio hayo jana wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa Government City Complex  katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba unaogharimu  kiasi cha shilingi Bilioni 59.3 hadi kukamilika kwake ambapo ametumia nafasi hiyo kulipongeza jiji la Dodoma kwa kutekeleza kwa kutumia mapato yake ya ndani na si fedha za serikali.

Amesema hakuna halmshauri yoyote iliyofanya uwekezaji mkubwa nchini kama uliofanyika katika Jiji la Dodoma huku akieleza kuwa sasa analiona jiji hilo kupitia viongozi wake kuwa wapo kwenye sura hiyo anayoitamani.

“Hakuna halmashauri yoyote iliyofanya uwekezaji mkubwa  kama huu hivyo nawapongeza jiji la Dodoma, nataka  jengo hili liwe kielelezo na kama nilivyosema mimi matamanio yangu nataka nione halmashauri zinazoweza kujitegeme zenyewe ifike muda halmashauri iseme hata nikiwa na watumishi wangu nitawalipa mimi mwenyewe natamani itokee ndani ya miaka mitatu ijayo,” amesema  Waziri Jafo.

Ameendelea kufafanua kuwa  analiona Jiji la Dodoma lipo kwenye sura hiyo kupitia hoteli hiyo kubwa ya mikutano iliyojengwa katika Mji wa Serikali.

“Nikiangalia hoteli kubwa ilivyo kuwa mjini ya ghorofa 11 nikiangalia soko lenu la Dodoma nikiangalia eneo la maegesho ya magari Nala, eneo la mapumziko na michezo Chinangali, Stendi ya Dodoma, ninapata uhakika kwamba halmashauri ya jiji la Dodoma inaenda kujitegemea,”amesisitiza Waziri Jafo.

Ameuagiza uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha wanakwenda kusimamia kazi hiyo kwa kiwango cha juu ili iwe nzuri ambapo  mtu akija ajifunze  na kumtaka mkandarasi  kutulia na kufanyakazi kwa uangalifu mkubwa.

Amesema anahitaji jengo hilo kuwa kielelezo na kama nilivyosema mimi matamanio yangu ni kuona halmashauri zinazoweza kujitegemea zenyewe na ifike wakati ziwe zinalipa wafanyakazi wake kupitia fedha za ndani”

Amemuagiza mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na mshauri wa mradi huo anayehusika na kazi ya michoro kuhakikisha ifikapo siku ya jumatatu awe amekamilisha kazi na asiwe kikwazo cha kuchelewesha mradi.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa Jiji Joseph Mafuru amesema mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi  Bilioni 59.3 ambapo kwa awamu mbili ambapo ya kwanza ni ujenzi wa jengo la Tower B lenye ghorofa tano na kumbi za mikutano tano zenye uwezo wa kuchukua watu 1297.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.