• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Jafo awatunuku Tuzo Wanafunzi 4191

Imewekwa tar.: October 31st, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewatunuku wanafunzi 4191 tuzo za Astashahada ya awali, kati na Stashahada za chuo cha Serikali za Mitaa  mapema leo Tarehe 31/10/2019 katika viwanja vya Magufuli Square vilivyopo Hombolo chuoni hapo.

Akiwa katika Mahafali hiyo Waziri Jafo amewataka wanafunzi hao kwenda kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili waweze kutangaza sifa njema ya Chuo cha Serikali za Mitaa.

“Najua wengi hapa mtaajiriwa na mtaajiriwa katika Halmashauri zetu nataka muende mkazitendee haki halmashauri hizo, mkafanye kazi kwa bidii na kuleta mabadiliko chanya katika mamlaka zetu za Serikali za Mitaa”

Chuo hiki kinatoa maarifa stahiki kwa mahitaji ya soko la ajira la sasa,  napokea sifa nyingi za wahitimu wa chuo hiki wanapofanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini, naamini ninyi mnaohitumu leo mmeiva vyema kwenda kulitumika Taifa hili alisema Jafo.

Aliongeza kuwa Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma ukawe muongozo wenu katika utendaji kazi wenu wa kila siku, mkafanye kazi kwa umakini mkubwa ili tuzidi kuwa na wataalamu wenye weledi  ili maendeleo ya Taifa yaweze kufikiwa.

Wakati huo huo Waziri Jafo amezitaka  Halmashauri zote kuanza kutumia mfumo ulioboreshwa wa fursa na vikwanzo kwa maendeleo ambao umeandaliwa na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kwa kushirikiana na JICA.


“Mfumo huu ulioboreshwa utazisaidia Halmashauri zetu katika kupambana na vikwanzo vya maendeleo na kuona ni namna gani zinaweza kutumia fursa zinazopatikana katika maeneo hayo” Alisema Jafo.

Nikipongeze chuo hiki kwa kuwa wabobezi na mahiri katika maandiko yenye kutoa Dira na muelekeo  wa kupambana na changamoto zilizoko katika Mamlaka za Serikali za Mitaa alimalizia Jafo.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Mpamila Madale amesema chuo hicho mbali na kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi pia wamejikita katika Tafiti, kutoa ushauri wa kitaalam pamoja na kuandaa machapisho ya kitaaluma.

Alisema mpaka sasa chuo cha Serikali za Mitaa  kina jumla ya wanafunzi 7436 na ongezeko la wanafunzi hao kumepelekea uhaba wa madarasa ambapo kwa mwaka huu wameweza kujenga darasa moja lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 504 kwa kutumia mapato ya ndani na ujenzi huo umetumia  force account.

Mahafali haya ni mahafali ya kumi na moja na yamehudhurisha wahitimu wa Astashahada ya awali ya ugavi na manunuzi, menejiment ya rasilimali watu,utunzaji wa kumbukumbu, pamoja na maendeleo ya jamii.

Wanafunzi walohitimu kwenye Astashahada ya kati ni Utawala katika Serikali za Mitaa, Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa, Ugavi na manunuzi,menejiment ya rasilimali watu, utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka na Astashahada ya kati ya maendeleo ya jamii;

Wakati huo huo wanaofunzi waliohitimu katika ngazi ya Shahada ni Utawala katika Serikali za Mitaa, Uhasibu na Fedha katika Serikali za Mitaa, Menejiment ya Rasilimali watu, Maendeleo ya jamii, Ugavi na manunuzi pamoja na Stashahada ya Utunzaji wa Kumbukumbu 2019.



Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA KUSUKWA UPYA

    January 23, 2023
  • MAKAMU WA RAIS AWAPONGEZA DODOMA JIJI KWA UWEKEZAJI

    January 20, 2023
  • SERIKALA YASISITIZA KILA MMOJA KUTUNZA MAZINGIRA

    January 20, 2023
  • TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKANA NA WADAU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    January 20, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.