• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

Jafo awataka watumishi wa umma kujiunga Benki ya Walimu

Imewekwa tar.: March 11th, 2021

Na Atley Kuni, DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo (Mb), amewataka watumishi wa kada ya ualimu na watumishi wengine wa umma kujiunga na Benki ya Biashara ya Walimu ijulikanayo kama ‘Mwalimu Commercial Bank’ ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na benki hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya kadi za Viza, Mwalimu Mobile na Mwalimu Wakala, Mhe Jafo amesema umefika muda kwa maafisa masoko wa benki hiyo, kuwatembelea watumishi walimu na wasio walimu kwa ajili ya kuwashawishi waweze kujiunga na benki ya Mwalimu.

Amesema walimu wengi wakijiunga na huduma za benki hiyo kutaiwezesha kukuwa zaidi, kwani kundi hilo linakadiriwa kuwa na watumishi laki tatu ambao ni asilimia 72.6 ya watumishi wote wa umma

“Kutokana na wingi wenu huu lazima muone ipo haja sasa ya kujiunga kwa wingi, lakini msiishie hapo tu, bali pia wafikieni watumishi wengine wa kada zingine, nalisema hili kwani najua nguvu ya walimu ni kubwa na hakuna la kuwashinda,” amesema.

Waziri Jafo amekumbusha kuwa malengo ya kuanzishwa kwa benki hiyo yalikuwa ni kuwahudumia walimu kama wateja wao wakuu lakini kufikia sasa idadi ya walimu waliojiunga kupata huduma za benki ni 41,000 tu.

“Hapa maafisa masoko bado mna kazi kubwa ya kujenga uelewa wa pamoja ili watu wafahamu kwamba hiki ni chombo chao” amesema.

Akizungumzia kuhusu huduma mpya zilizoanzishwa na benki hiyo, Waziri Jafo amesema kuanzishwa kwa huduma hizo ni ishara kuwa huduma zitolewazo na benki hiyo zimeongezeka, hivyo ni jukumu la uongozi wa benki hiyo kuongeza hamasa na ushawishi kwa walimu na watumishi wengine wa umma kujiunga ili kufaidi huduma za benki hiyo.

“Uanzishwaji wa huduma hizi, ni ishara kwamba mmeongeza wigo, hata mtu ambaye alikuwa anasita kujiunga na benki yenu, sasa mmempatia suluhisho kwani kupitia huduma kama ya Mwalimu Mobile, mtu ataweza kufanya muamala eneo lolote lile alipo, hivyo tumieni mwanya huo kuwahamasisha walimu na watumishi wengine kujiunga zaidi,” amesema.

Waziri Jafo amesema kutokana na huduma za benki hiyo kutokuwa karibu na maeneo wanayofanyia kazi walimu hasa maeneo ya vijijini,  baadhi ya walimu wanalazimika kuziacha kadi zao kwa taaasisi binafsi zinazotoa huduma za kifedha ili waweze kukopa mikopo mbali mbali, hivyo akaitaka benki hiyo kusogeza huduma karibu na walimu ili kuwawezesha kupata huduma ya benki hiyo.

Pia Waziri Jafo, ameitaka Bodi ya Benki ya Mwalimu kuona kwa namna gani wataweza kutoa mikopo kwa riba shindani na kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo ya Nyumba kwa wateja wao  ili iwe kichocheo cha wateja wengi zaidi kujiunga katika benki hiyo.

Awali akitoa salamu kabla ya kumkaribisha Waziri Jafo, Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Walimu Francis Ramadhan, amesema benki hiyo inazidi kuboresha huduma zao kwani tayari wana ofisi katika Mikoa ya Mbeya, Morogoro na Mwanza pamoja na sehemu za huduma zipatazo 2000 nchini kote pamoja na kuanzisha huduma ya Bima kwa wateja wake.

Mwalimu Commercial Bank, ilianzishwa mwaka 2012, na inamilikiwa na Chama cha Walimu kwa asilimia 51 ya hisa, huku wadau wengine ukiwemo Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) ambao unamiliki asilimia 16 na asilimia nyingine zilizosalia zinamilikiwa na  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NIHF na wadau wengine.

Picha za Viongozi mbali mbali wakati wa hafla hiyo

Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • BARABARA YA MVUMI KUWEKWA LAMI KM 3

    May 26, 2022
  • PROF. SHEMDOE AZINYOOSHEA KIDOLE HALMASHAURI 8 KWA KUTOKUTENGE FEDHA ZA LISHE

    May 25, 2022
  • WAZIRI MKUU MAJALIWA ASIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA JIJI, MAAFISA WATANO ARUSHA

    May 24, 2022
  • WAKUU WA MIKOA SIMAMIENI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE HALMASHAURI

    May 24, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.