• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Jafo atoa maagizo mazito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

Imewekwa tar.: June 3rd, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga kumrejesha aliyekuwa afisa manunuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.

Ametoa maagizo hayo leo wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wakati akiwa kwenye ziara ya  kikazi ya  kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa  katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

Mhe. Jafo ameyasema hayo baada ya kubaini ubadhilifu wa fedha za Serikali uliofanywa na Afisa huyo ambaye alihamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na kuhamishwa kituo kingine cha kazi.

Amemwagiza Mhandisi Nyamhanga kuunda tume ya uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha za serikali kwa mtumishi hiyo ambaye kwa sasa amehamishwa kwenda kituo kingine cha kazi na tume hiyo itatoa taarifa na ushauri wa kufanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi

“Haiwezekani mtumishi afanye  ubadhilifu wa fedha za Serikali kisha ahamishwe kituo cha kazi, huo si utaratibu, Ninamuagiza Katibu Mkuu kutengua uhamisho huo na kurejeshwa kwenye kituo cha awali ili kujibu tuhuma” Amesisitiza Mhe. Jafo

Amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imekuwa ikisuasua katika utekelezaji wa  miradi ya maendeleo kutokana na uzembe  wa baadhi ya watumishi katika kutekeleza majukumu yao jambo ambalo  linarudisha nyuma  juhudi za Serikali za kuleta maendeleo kwa jamii.

Mhe. Jafo anafafanua kuwa baadhi ya watumishi wanaopatiwa dhamana ya wanatumia madaraka waliyonayo kinyume na utaratibu  na kupelekea kutotenda haki kwa wananchi jambo ambalo linaongeza malalamiko kwa wananchi watunaowahudumia.

“Viongozi tunaopewa dhamana na wananchi, tutende haki, tuache majivuno na tuache kudharau watumishi wengine bali  fanyeni kazi kwa kufuata Sheria, Taratibu na miongozo ya kiutumishi wa umma lengo likiwa ni kutoa huduma bora kwa jamii” Amesisitiza Mhe. Jafo.

 Mhe. Jafo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha takukuru wanafanya uchunguzi wa kina kubaini tatizo la ubadhilifu wa fedha za umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.

Aidha, Mhe. Jafo amewataka watumishi kufanyakazi kwa uadilifu kwa kufuata sheria, taratibu  na miongozo ya kiutumishi wa umma  kwa kufanya hivyo kutapunguza malalamiko na kuziletea maendeleo Halmashauri zote nchini.

Akizindua nyumba za watumishi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda Mhe. Jafo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  kwa kuhakikisha wanajenga nyumba za watumishi kwa kutumia Force Account jambo ambalo limesaidia kupunguza gharama katika ujenzi huo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha Mkoa wa Katavi unafikika kwa kujengewa miundombinu ya barabara na Stendi hali iliyoleta mabadiliko makubwa katika kukuza uchumi wa wananchi na Mkoa kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Jafo yupo kwenye ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kitavi kukagua miradi inayotekeleza katika Halmashauri ya Manispaa ya Katavi ambapo amezindua nyumba za watumishi, kutembelea ujenzi wa  ofisi ya Mkoa wa Katavi na ukaguzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 7.7 zilizojengwa chini ya mradi wa Uendelezaji Miji (ULGSP)

Na. Angela Msimbira KATAVI


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.