Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

JAFO asema siku tisa zilizobaki ni lazima miradi ikamilike

Imewekwa tar.: February 6th, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuhakikisha ujenzi wa Miradi ya soko na stendi Dodoma inakamilika ifikapo Februari 15, 2020 kama Rais Dkt John Magufuli alivyoelekeza.

Ametoa maagizo hayo leo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo inayojengwa kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji Mkakati Tanzania (Tanzania Strategic Cities Project) inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.  

Mhe. Jafo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi wa mradi huo alimwagiza mkandarasi anayetekeleza miradi hiyo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi ifikapo Februari 15, 2020, hivyo ni wajibu wa mkandarasi huyo kutimiza maagizo hayo kwa wakati uliotolewa.

Amesema kuwa ameridhishwa na kiwango cha ujenzi uliofanyika katika miradi hiyo, kwa kuwa mkandarasi huyo ameonyesha uzalendo wa dhati wa kujenga majengo yenye uimara wa hali ya juu lakini hadi kufikia februari, 15, 2020 wahakikishe wamekamilisha kazi na majengo hayo yanaanza kutumika.

“ Nimeridhishwa na ujenzi wa miradi hii ya Soko na stendi ya mabasi, kwa kuwa vimejengwa  kwa uimara mkubwa,hasa katika umaliziaji wa majengo, na ubora wa kazi uliofanyika lakini nasisitiza kuhakikisha  kazi hiyo inakamilika kwa muda uliopangwa” amesisitiza Mhe. Jafo

Amemuagiza mkandarasi Mohamed Builders  kuhakikisha wanaongeza nguvukazi na kufanya kazi usiku na mchana ili kuweza kukamilisha kwa wakati na wananchi wa Mkoa wa Dodoma waweze kupata huduma bora na kwa wakati uliopangwa.

Wakati Huohuo, Mhe Jafo ameuagiza uongozi wa Halmashauri wa Jiji la Dodoma kuhakikisha wanaweka mikakati bora ya usimamizi  na uendeshaji wa miradi hiyo ili  kulinda ubora wa stendi na soko ili kuepusha lawama zitakazojitokeza wakati wa kutoa huduma katika maeneo hayo.

“Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi hakikisha unaweka mikakati mizuri ya uendeshaji na usimamizi wa miradi hii ili kupunguza malalamiko kwa wafanyabishara na watoa huduma katika eneo hili na pia kulinda miundombinu na usafi wa maeneo hayo” Ameagiza Mhe. Jafo

Ameeleza kuwa Serikali imetumia gharama kubwa katika ujenzi wa Miradi hiyo, lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma wanakuza uchumi na kujiongezea kipato, hivyo ni wajibu wa Halmashauri kuhakikisha wanaweka mikakati bora ya jinsi ya kuendesha miradi hiyo.

Amemtaka kuhakikisha Halmashauri inakusanya mapato kwa wakati lakini  waangalie gharama rahisi watakaotoza wananchi ili kupunguza lawama zinazoweza kujitokeza katika uendeshaji wa miradi hiyo.

“Halmshauri ya Jiji la Dodoma kusanyeni mapato ili kuongeza uchumi lakini watozeni wafanyabishara gharama inayokubalika, isijesababisha miradi hii kukimbiwa na wananchi wakiogopa gharama zinazotolewa na Halmashauri ya Jiji na kuifanya kukaa bila kutumiwa kwa lengo lililokusudiwa na Serikali”amesema Mhe Jafo

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema kuwa tayari Ofisi yake imeunda kamati maalumu kutoka Wizara ya fedha, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Jiji kwa kuweka uwazi na timu imeanza kazi,kamati ikimaliza kazi yake watatangaza watu waje kupangisha na  kampuni ya jiji la Dodoma City Investment Company itakuja  kufanya kazi ya operesheni.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.