• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali

JAFO alia na riba kubwa za mikopo zinazotolewa na mabenki nchini

Imewekwa tar.: August 22nd, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe, Selemani Jafo amesema kuwa suala la mikopo wanayopewa waalimu na watu mbalimbali  nchini na  taasisi za kifedha zimekuwa ni  changamoto jambo ambalo linawasababisha kutokupata maendeleo stahiki na kuwa na madeni makubwa ambayo yanawasababishia umaskinii

Ameyasema hayo wakati akifungua siku wa waalimu kupitia benki ya NMB iliyofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo ameiomba benki ya NMB nchini kuhakikisha wanafanya utafiti wa kuwatambua wateja ambao ni wafanyakazi hasa Waalimu wanapatiwa mikopo yenye riba nafuu ambayo itawasaidia katika kujiongezea kipato na kujipatia maendeleo binafsi.

Ameendelea kufafanua kuwa benki hiyo inahitaji kuweka mikakati ya kuwasaidia waalimu pindi wanapokopa katika taasisi za kibenki kwa kuwapunguzia riba hadi kufikia digiti moja jambo ambalo litawafanya waalimu wengi kupata fursa ya kukopa na kujiendeleza kiuchumi.

Amesema lengo la mikopo ni kuwasaidia waalimu ili wajikwamue kiuchumi hivyo kwa kuweka riba kubwa kunasababisha waalimu wengi nchini kubaki maskini na kujikuta wanakopa kila mahali kutokana na fedha yote ya mshahara kuishia kwenye kulipa mikopo.

“Waalimu wakiajiriwa wanauhakika na ajira hiyo hadi kustaafu hivyo akikopa benki inauhakika na mteja huyo, sasa kwa nini riba ya mwalimu inakuwa sawasawa na mfanyabishara mkubwa au mfanyakazi ambaye ameajiriwa kwa mkataba, ninawaomba benki ya NMB mliangalie hilo ili waalimu wengi wajikwamue kiuchumi”Amesema  Mhe.Jafo

Amesema kuwa watumishi wengi wakiwemo waalimu wamekuwa wakiteseka na mikopo ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi za kibenki jambo ambalo linasababisha malengo ya kufikia uchumi wa kati kuwa ni ndoto kwa watumishi wengi nchini.

“Ikifika tarehe 21 kila Mtumishi akiwemo mwalimu nchini kichwa kinamuuma kwa kuwa mshahara unakuwa umetoka lakini madeni aliyonayo yanazidi mshahara uliowekwa benki jambo ambalo linawafanya waalimu wengi kubaki maskini kila siku na kuwa watumwa wa mikopo” Amesema Mhe. Jafo.

Mhe. Jafo anafafanua kuwa Mikopo inawasaidia wananchi na hasa waalimu lakini bado wanateseka na riba kubwa zinazotolewa na mabenki jambo ambalo linawaumiza na kuwa watumwa wa kulipa madeni na sio kujikwamua kiuchumi.

Wakati huohuo Mhe. Jafo ametoa onyo kwa waalimu nchini kuacha kukopa mikopo kwa tamaa bali wakope kwa malengo ili kutimiza malengo yao ya kujiongezea kipato

“Waalimu wanaenda kukopa kwenye Sacoss hadi kadi zao za benki zinaachwa huko, mwalimu anatoa mpaka namba ya siri ya kadi yake ili mshahara ukiingie akatwe mkopo,hii si vizuri hata kidogo kwani waalimu wanadhalilika mitaani ” Amesema Mhe. Jafo.

Amewataka waalimu kuacha tamaa, bali waishi kulingana na kipato unachokipata, kwa kuwa kinachotokea baada ya kuwa na mikopo mingi ni waalimu wengi kudhalilika katika jamii

Aidha Mhe. Jafo ameitaka  benki ya NMB kuja na mkakati wa kuwasaidia waalimu katika kujikwamua kiuchumi na kujiongezea mapato lengo likiwa ni kupunguza umaskini nchini.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI




Matangazo

  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Taarifa ya Kitengo Manunuzi na Ugavi, April 2022 April 04, 2022
  • Safeguard Documents for TACTIC Project March 30, 2022
  • Miongozo ya Operesheni Anwani za Makazi March 24, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU MASHULENI KUPITIA MEWAKA

    May 19, 2022
  • Bashungwa apongeza ongezeko la Mishahara kwa watumishi nchini

    May 18, 2022
  • WALIMU WAMEIOMBA SERIKALI KUENDELEA NA MAFUNZO YA MEWAKA

    May 17, 2022
  • BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA - GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

    May 14, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.