• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Hospitali ya Mabwepande yatakiwa kutoa huduma za afya ifikapo Desemba 30, 2021

Imewekwa tar.: November 24th, 2021

Na Fred Kibano, Dar es Salaam

Serikali imeagiza kukamilika kwa miundombinu ya hospitali mpya ya wilaya ya Kinondoni Mabwepande ifikapo tarehe 30 mwezi Desemba mwaka huu na kuanza kutoa huduma zote za afya kwa wananchi.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Dkt. Festo Dugange Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI alipofanya ziara yake mapema hii leo Jijini Dar es Salaam na kukuta hali ya kusuasua kwa ujenzi wa baadhi ya majengo mbali na Serikali kupeleka zaidi ya shilingi Bilioni tatu kwa awamu tofauti.

Dkt. Dugange amesema haiwezekani kwa takribani miaka nane sasa hospitali hiyo iwe haijakamilika na wananchi wanapata shida ya kupata huduma za afya mbali na maeneo hayo wakati Serikali imewekeza fedha kwenye hospitali hiyo shilingi Bilioni tatu na milioni mia nne.

Dkt. Dugange amewaagiza watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam na Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha majengo mama na mtoto, maabara, jengo la mionzi, chumba cha kuhifadhia maiti, na jengo la upasuaji, jengo  la kutolea dawa na stoo ya dawa kukamilika mapema iwezekanavyo na kuanza kazi ifikapo Tarehe 30 Desemba, 2021.

“majengo yote ya mama na mototo, wagonjwa wa nje, huduma za upasuaji na kulaza wagonjwa miundombinu yote ikamilike kwa wakati na muanze kutoa huduma zote ifikapo Desemba 30, mwaka 2021”

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuchukua hatua za kinidhamu kwa wale wote walioshindwa kusimamia ujenzi wa jengo la ghorofa nne la hospitali ya wilaya Mabwepande kwa kuwa na kasoro zinazofanana kuanzia ghorofa ya kwanza hadi ya nne na wasimamizi wa kazi hiyo wapo na pia kuhakikisha taarifa ya kutoa adhabu kwa watumishi hao inawasilishwe Ofisi ya Rais TAMISEMI mara moja.

Kwa upande wake Dkt. Rashidi Mfaume ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesema maelekezo yote wamezingatia na kwamba kwa sasa wasimamizi wa ujenzi wa hospitali ya Mabwepande watapiga kambi katika hospitali hiyo mpya yenye hadhi ya Wilaya ili kukamilisha majengo yote na kuanza kutoa huduma maramoja ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2021.

Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Samwel Laizer amesema wamezingatia maelekezo yaliyotolewa na kwamba mwishoni mwa mwezi Desemba 2021 wataanza kutoa huduma za afya maramoja.


Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.