Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Halmashauri Zijiandae Kukabiliana Na Ugonjwa wa Pumu

Imewekwa tar.: May 11th, 2019

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amezitaka halmashauri kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya visanduku vya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu katika shule zote za msingi na sekondari.

Pia amesema ni lazima wakurugenzi katika halmashauri zote kuwa na visanduku huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu na mengineyo katika ofisi zao jambo ambalo litawasaidia wafanyakazi wenye matatizo hiyo kupewa huduma ya kwanza kabla ya kufika hospitalini.

Jafo alitoa maagizo hayo jijini hapa baada ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Pumu Duniani ambayo huadhimishwa Mei 7 kila mwaka.

Alisema tatizo la pumu ni kubwa na takwimu zinaonesha kuwa nusu ya watu wenye pumu ni watoto ambao wengi wako mashuleni na hawana uwezo wa kujisaidia.

“ Ukiangalia takwimu za Shirikala afya zinasema vifo vinavyotokana na pumu hapa nchini ni zaidi ya 2,000, sasa kama nusu ya hao ni watoto  hii inamaanisha tunapoteza shule mbili nzima, yaani wanafunzi wa shule iliyokamili kutoka Darasa la Kwanza hadi la Saba. Hii inaonesha tatizo hili ni kubwa na kama taifa tunahaja ya kutathimini kama taifa.”

Kutokana na hali hiyo, Jafo aliagiza halmashauri katika bajeti ya mwaka 2020/2021, halmashauri zitenge fedha Sh laki 100,000 kwa kila shule katika eneo lake ili kununua visanduku viwili vya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu.

“ Ghamara ya first aid kit moja ya huduma ya kwanza kwa ugonjwa wa pumu ni Sh 50,000 hivyo kila shule ikitengewa kits mbili haitakuwa fedha kubwa, Hivyo kwa shule zote  zaidi ya 17,000 kutenga Sh bilioni 1.7 kwa hili sio fedha nyingi. Maadamu bajeti imeshipata, tutakapoanza maandalizi ya bajeti nyingine, halimashauri iliingize hili.”

Jafo alisema jamii kubwa ya Watanzania haina ufahamu wa tatizo la ugonjwa wa pumu, dalili na namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa wa aina hii hivyo aliwataka maadhimisho hayo kupewa kipaumbele kwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yao kuadhimisha siku hii kwa kutoa elimu katika jamii na mashuleni.

Pia aliaziagiza halmashauri na mipango miji kutenga maeneo kwa ajili ya mazoezi ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukizo, akiutaka mkoa wa Dodoma kuangalia namna ya kutenga siku moja kwa mwezi kwa walimu na wanafunzi kushiriki katika mazoezi

Jafo pia alisema kwa kushikiana na wizara nyingine wataangalia namna ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhudumia magonjwa yasiyoambukiza na kuangalia namna ya magonjwa haya kuingizwa kwenye mitaala ya elimu ili wanafunzi wapate elimu ya awali kama ilivyo kwa HIV.

Aidha, Jafo aliwapongeza waandhaaji wa madhimisho hayo kwa kazi ya kuwafundisha walimu 40 ambao wamepewa mafunzo ya namna ya kutoa huduma kwa wananfunzi wenye ugonjwa wa pumu na kushauri toa mafunzi kwa walimu wa walimu na kushauri wigo wa kufundisha walimu hao kuo

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Magonjwa ya Mfumo wa Hewa (TARD) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukuzia(Tancida), Dk Digina Riwa alisema takwimu za WHO zinaonesha dunia inawagonjwa zaidi ya milioni 3 huku nusu ya wagonjwa hao ni watoto.

Alisema kwa Tanzania tawkimu hizo zinaoneshwa kuwa vifo 2,491 vinatokana na ugonjwa wa pumu na kuwa kutokana na makadirio ya kuwa wagonjwa wa pumu wanaweza kuongezeka kwa asilimia 30, Shirikisho hilo likajikita katika kutoa elimu.

Akizungumzia sababu ya maadhimisho hayo jiji Dodoma,  Riwa alisema ni baada ya kubaniki kuwapo kwa tatizo hilo na kutoa takwimu kuwa kwa mwaka jana pekee wilaiaya ya Mpwapwa ilikuwa na wagonjwa 1,223, Kongwa ni 1,101, Chemba ni 1,459 na Chamwino wagonjwa 1512.

Alisema katika kuadhimisha mwaka huu wameamua kufanya upimaji katika shule za msingi na sekondari ambao wameweza kuwapata wale ambao wanajitambua kuwa na ugonjwa, lakini idadi kubwa ya wanafunzi walikuwa wahajitambui.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bahi na ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mwanahamisi Mukunda alihidi kuwa mkoa utaedeleza mkakati wa kutambua na kubaini watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa pumu.

“ Kwetu sisi mmetusaidia kubaini ukubwa wa tatizo, tumekuwa hatufanyi vizuri kwenye ufaulu kwenye mitihani ya taifa na tulikuwa tunatafuta mchawi, kumbe mmoja wa mchawi ni tatizo la pumu ambalo linachangia wanafunzi kukosa masomo.”alisema


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • RC CHALAMILA ATAKA MACHINGA KARIAKOO KUFUNGUA NJIA

    May 30, 2025
  • Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana watakiwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.

    May 29, 2025
  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.