• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Halmashauri zarejeshewa kukusanya ushuru wa Majengo, Mabango

Imewekwa tar.: February 1st, 2021

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwanaidi Ally Khamis, wakati wa kikao hicho

Na Atley Kuni, Dodoma

SERIKALI imesema kuanzia sasa ushuru wa majengo, mabango na vitambulisho vya Wajasiriamali umerejeshwa rasmi kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa, isipokuwa ule unaosimamiwa na TANROAD na TARURA.

Tamko hilo limetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwanaidi Ali Khamis wakati walipozungumza na waandishi wa Habari.

Wamesema lengo la kurejesha ushuru huo ukusanywe na Halmashauri ni kuongeza wigo mpana wa kukusanya mapato yake ili kupitia vyanzo hivyo ili kuiwezesha Serikali kutekeleza shughuli mbali mbali za maendeleo.

Akizungumza kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari, Waziri Jafo alisema kuanzia sasa ushuru wa majengo, mabango na vitambulisho utakusanywa na halmashauri kama awali isipokuwa ule unaosimamiwa na TANROAD na TARURA.

Alisema kutokana na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwa na Mtandao mpana ambao umekwenda hadi katika ngazi za vijiji, mitaa na vitongoji, na kwa kuwa zipo karibu na kutambua mabango ni dhahiri zitaweza kukusanya ushuru wa mapato kwa urahisi Zaidi.

“Hivyo nitumie fursa hii, kuwataka Wakurugenzi wote kupitia, Maafisa biashara, maafisa Kata, na Vijiji waweze kukusanya kodi kwa kuwafikia wafanya biashara wote katika maeneo yao,” alisema Waziri Jafo.

Aliongeza kuwa kutokana tamko hilo hatarajii kuanzia sasa kuona kuna mfanyabiashara anayefanya biashara bila kulipa kodi ya mapato ya TRA, leseni ya biashara ya Halmashauri au bila kitambulisho cha wajasiliamali na kuonya kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaofanya biashara zao kinyume na agizo la serikali.

Kuhusu vitambulisho vipya vya wajasiliamali Waziri Jafo alisema vitambulisho hivyo tayari vimekwishachapishwa na kupelekwa katika ofisi za TRA nchini kote na sasa vitakuwa chini ya Wakuu wa Mikoa hivyo, Wakurugenzi wa Halmashauri wanapaswa wakachukue tayari kwa kuwafikishia wajasiriamali.

Amesema, vitambulisho vilivyoboreshwa vitapatikana kwa bei ile ile ya shilingi elfu ishirini (20,000) kwa kitambulisho kimoja ambapo mfanyabiashara ataweza kufanya biashara zake mwaka mzima bila kubugudhiwa.

Aidha Waziri Jafo amewaonya baadhi ya wafanyabiashara wa maduka makubwa wasiokuwa waaminifu wanaowapatia bidhaa wajasiriamali wadogo, kuacha mara moja tabia ya kuwapatia bidhaa wajasiriamali wadogo ili wakatembeze mitaani kwa lengo la kukwepa kodi.

“Mfanyabiashara yoyote anayefanya hivyo ni mhujumu uchumi kupitia mapato, kama walivyo wahujumu chumi wengine, hivyo Serikali haitamfumbia macho na badala yake mkondo wa sheria utachukua nafasi yake, ni rai yangu kila mtu anayeuza bidhaa, atoe risiti na kila anayenunua bidhaa adai risiti,” Mhe. Jafo alisisitiza.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa fedha Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, ambaye alizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha amesema, serikali ya awamu ya tano imeendelea kulipa uzito suala la kulipa kodi kama ajenda ya kudumu ambayo inatajwa na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi-(CCM) 2020/2025.

Akiongea kwa njia ya simu kutoka wilayani Magu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Lutengano George Mwalwiba, alipongeza hatua ya serikali kuwarejeshea kukusanya vyanzo hivyo vya mapato kwani mtandao wa Mamlaka hizo ni mpana ikilinganishwa na taasisi zingine.

Ushuru wa huo uliondoshwa katika mamlaka hizo mwaka 2018 na kukabidhiwa Wizara ya Fedha chini ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA, hata hivyo katika kile kinacho onekana kuzidisha wigo wakukusanya Mapato, Serikali imeamua, kazi hiyo kurejeshwa tena kwenye mamlaka hizo ili kuongeza tija na ufanisi.

Baadhi ya watumishi kutoka Ofsisi ya Rais-TAMISEMI, wakiwa wanafatilia mkutano huo

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo

Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • TUNZENI VIFAA VYA AFYA VILIVYONUNULIWA NA SERIKALI - DKT. MAHERA

    March 30, 2023
  • REJESHENI MIKOPO ILI WENZENU WAPATE KUKOPA –KAMATI YA LAAC

    March 31, 2023
  • LAAC YARIDHISHWA NA USIMAMIZI WA UKARABATI SHULE YA SEKONDARI WASICHANA MTWARA

    March 31, 2023
  • KAMATI YA LAAC YAKAGUA MADARASA 7 YALIYOJENGWA KWA MAPATO YA NDANI NA NGUVU ZA WANACHI - MANISPAA YA SUMBAWANGA

    March 31, 2023
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.