• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Halmashauri zaagizwa kutenga viwanja vya michezo

Imewekwa tar.: June 10th, 2019

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri za majiji na miji nchini kuhakikisha kuwa zinatenga maeneo ya michezo na burudani kila zinapopima viwanja.

Akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za msingi na sekondari Tanzania, katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara leo, Waziri Mkuu amesema kuwa halmashauri zina wajibu mkubwa wa kuweka mpango madhubuti wa kuyaendeleza maeneo yote ya michezo na burudani.

Amesema ifikapo Septemba 30, 2019, kila halmashauri iwe imefanya mapitio ya maeneo yote yaliyokuwa yamepimwa kwa matumizi ya huduma maalum ikiwemo michezo, burudani, shule na ibada na kutoa taarifa kama yanatumika kwa ajili hiyo au vinginevyo.

“Naagiza kuanzia sasa, maeneo yote yanayopimwa na halmashauri na miji yote nchini, lazima yazingatie uwepo wa maeneo ya michezo na burudani,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Amesema katika baadhi ya maeneo kumekuwepo na uhaba wa viwanja vya michezo kwa sababu ya mipango miji isiyozingatia mipango endelevu ya sekta mbalimbali.

Hivyo, Waziri Mkuu ameagiza yafanyike marekebisho na hatua za haraka ili kutoa fursa ya ukuaji wa michezo na kusaidia wananchi kushiriki michezo, mazoezi na kupata burudani.

Akizungumzia kuhusu mashindano ya mwaka huu ambayo yameshirikisha wanafunzi wengi zaidi wenye mahitaji maalumu, Waziri Mkuu amesema waendelee kuwahusisha wanafunzi wote katika michezo, sanaa na burudani bila kujali aina ya ulemavu walionao.

Amesema jambo hilo ni muhimu kwa kuwa vipaji vipo kwa wote na fursa ndizo zitakazowawezesha kuonesha vipaji hivyo na kuvikuza.

Waziri Mkuu amewasisitiza wadau wote wa shule za msingi, sekondari, vyuo, sehemu za kazi na wizara, waweke mipango ya kudumu ya kuwashirikisha watu wenye mahitaji maalumu katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi bila ubaguzi wowote.

“Hakikisheni baadhi ya vikwazo katika kushirikisha watu wenye mahitaji maalumu kwenye michezo vinaondolewa. Vikwazo hivyo ni pamoja na kutokuwepo kwa mipango endelevu katika maeneo mbalimbali na uwepo wa mitazamo hasi ya baadhi ya walimu, wazazi na viongozi katika maeneo yao dhidi ya uwezo wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.”

Aidha, Waziri Mkuu ametuamia fursa hiyo kuupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuwa mmoja kati ya Mikoa ya mfano katika kutekeleza agizo lake la mwaka jana alilolitoa kupitia michezo hiyo la kuanzishwa kwa shule maalumu za michezo.

Mkoa wa Simiyu umejenga Shule ya Sekondari itakayokuwa kituo cha kukuza vipaji vya wanafunzi katika michezo. “Naagiza mwakani wanafunzi wote walioonesha vipaji katika michezo watakaofaulu Mtihani wa Elimu ya Msingi wapangwe katika shule hiyo ili wakakuze vipaji vyao,” amesema.

Amesema bila ya kuwa na mipango ya kulea na kukuza vipaji kutoka ngazi za chini Taifa haliwezi kupata mafanikio katika michezo nchini. Kwani katika kipindi ambapo michezo hiyo ilisitishwa kiwango cha michezo ya aina mbalimbali kilikuwa chini sana.

Mapema akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mashindano hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani jafo amesema kuwa lengo kuu la michezo hiyo ni kutekeleza azma ya Serikali ya kukuza sekta ya michezo kwa kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia wanafunzi shuleni.

“Michezo ni sehemu ya taaluma hivyo wanafunzi wanapata fursa ya kushindama, kuibua na kuviendeleza vipaji vyao na kujenga umoja wa kitaifa, upendo na mshikamano,” amesema.

Kauli mbiu ya michezo hiyo kwa mwaka 2019 inasema “ michezo na sanaa kwa elimu bora na ajira”

Ufunguzi huo pia  umehudhuriwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Maafisa Elimu kutoka mikoa yote nchini, walimu wa michezo pamoja na Maofisa wengine wa Serikali.





Ufunguzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Maafisa Elimu kutoka mikoa yote nchini, walimu wa michezo pamoja na Maofisa wengine wa Serikali.



Matangazo

  • Orodha ya waliopata vibali vya Uhamisho Septemba - Disemba 2022 (OR - TAMISEMI) January 21, 2023
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato cha Kwanza Waliorudia Mtihani January 15, 2023
  • Matumizi ya Lugha ya Kiswahili na Kingereza January 14, 2023
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2023 December 14, 2022
  • Orodha ya Waliopangwa kwenye Vituo vya Kazi Kada za Afya (Awamu ya Pili) Agosti 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • LAAC YAPOKEA TAARIFA KUHUSU UTAWALA NA UENDESHAJI WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

    March 14, 2023
  • SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MENDELEO, UKUSANYAJI NA UDHIBITI WA MAPATO KATIKA HALMASHAURI

    March 13, 2023
  • WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

    March 13, 2023
  • ACHENI KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA BARUA PEPE BINAFSI - DKT. MPANGO

    March 13, 2023
  • Angalia zote

Video

AJIRA MPYA 30,000 ZA UALIMU NA AFYA UHANDISI KUTANGAZWA 2023 SIKU HII
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.