Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Halmashauri tengeni asilimia 40 kwenye miradi, asilimia 10 kwenye vikundi kama inavyosema sheria - Dkt. Dugange

Imewekwa tar.: December 29th, 2021

Na Fred Kibano, Shinyanga

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema Serikali ilikwishapitisha sheria ya kuzitaka Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 40 ya makusanyo ya mapato yao kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini pia kutenga fedha za makusanyo yao asilimia 10 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu lengo likiwa kupeleka maendeleo kwa wananchi na Mamlaka husika.

Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki Dkt. Dugange ameupongeza mkoa huo kwa kuenga mapato yao ya ndani asilimia 40 kwa asilimia 92 hadi mwishoni mwa mwezi Novemba na kutaka mikoa mingine iige mkoa wa Shinyanga kwa kufikia malengo waliyojiwekea kwa kila robo mwaka.

“mara nyingi baadhi ya Halmashauri zimekuwa zikijisahau kupeleka asilimia 40 kwenye miradi ya maendeleo na Serikali imekuwa ikisisitiza ni lazima zile fedha ziende kwenye miradi yenye tija kwa wananchi”  alisema Dkt. Dugange.

Ameitaja baadhi ya miradi kwa sekta kuwa ni pamoja na barabara, elimu, afya, maji na mingineyo ambayo inaigusa jamii moja kwa moja.

Kuhusu mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ameziasa Halmashauri zote kutoa mikopo yenye tija kwa vikundi vichache ili viweze kuimarika kiuchumi na kuweza kurejesha fedha kwa wakati ili vikundi vingine vilivyofikia vigezo viweze kukopa pia kuliko kutoa fedha kidogo kwenye vikundi vingi ambayo haiweza kuwainua kiuchumi.

“jambo la msingi ni kuhakikisha sasa tunaboresha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 yenye tija, ni vyema ukawa na vikundi vichache lakini ukavikopesha fedha ambayo kimsingi itawawezesha kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine”  alisema Dkt. Dugange.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Sophia Mjema amesema yeye pamoja na viongozi wenzake watasimamia fedha za miradi ya maendeleo zikiwemo zile za asilimia 40 na zile za mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.

“tutahakikisha tunazisimamia fedha hizi vizuri na tutaendelea kuwaelekeza watu wetu” alisema Mheshimiwa Mjema.

Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bwana Chila Moses amesema Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga zimeendelea kupeleka fedha zinazotokana na mapato ya ndani kwa vyanzo visivyolindwa kwenye miradi ya maendeleo kwa wakati.

“hadi kufikia Novemba 30, 2021 kiasi cha shilingi 3,519,758,307 zimepelekwa kwenye miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, uwezeshaji wananchi kuichumi na barabara ambayo ni sawa na asilimia 92 ya makusanyo halisi ya shilingi 8,843,261,034.38” alisema Bwana Moses.

Aidha, Bwana Moses amesema katika  kipindi cha Julai hadi Novemba, 2021 mkoa wa Shinyanga umetoa mikopo isiyo na riba shilingi 93,846,247 kati ya shilingi 960,815,258 sawa na asilimia 97.19 ya makusanyo halisi kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Msovela: Fanyeni Kazi Kama Timu Kuleta Maendeleo

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.