Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

Halmashauri 5 zanufaika na mfuko wa kutatua changamoto ya uhifadhi wa wanafunzi mashuleni

Imewekwa tar.: October 2nd, 2021

HALMASHAURI za Wilaya tano nchini zimesaini makubaliano ya kutekeleza mradi wa changamoto ya uhifadhi wa Wanafinzi ili kuondokana na tatizo la mdondoko kwa wanafunzi.

Halmashauri hizo ni Bahi, Chamwino, Ruangwa, Kilwa na Liwale ambazo zitatekeleza mradi huo wa majaribio na unasimamiwa na taasisi ya Price Water Coopers (PWC) kwa ufadhili wa Dola za Marekani 500,000 kutoka Shirika la Maendeleo la Korea ya Kusini (KOICA).

Akizungumza jana kuhusu mradi huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof.Riziki Shemdoe, amesema Halmashauri 20 zilishiriki kuandaa andiko la mradi huo lakini baada uchambuzi wa maandiko hayo zilichaguliwa Halmashauri hizo tano.

Alisema mradi huo unalenga kubaini vikwazo vinavyosababisha wanafunzi wengi wa msingi na Sekondari kutomaliza masomo yao na kutafutia ufumbuzi.

“Niwapongeze sana kwenye hatua hii ya awali ya kushinda kuwa miongoni mwa Halmashauri tano zilizochaguliwa, nawashukuru sana wenzetu wa KOICA ambao ni wadau wa maendeleo bwana Kyucheol Eo ambaye ndiye Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA, amekuja kushuhudia kitendo hichi cha kusaini makubaliano haya ya kutekeleza mradi huu,”alisema.

Prof.Shemdoe alishukuru KOICA kwa kusaidia Tanzania kwenye sekta ya elimu kwa watoto waliopo Shule ya Msingi na Sekondari ambao wanapata vikwazo na kusababisha kufikia mwisho wa masomo yao.

“Kkwenye safari ya elimu kuna Shule za Msingi wanaanza vizuri kabla ya kufikia darasa la saba wanaanguka njiani, kuna changamoto nyingi wengine wanapata mimba wengine wanakuwa na sababu mbalimbali”

“Hivyo hivyo kwa wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza kwa mfano mwaka huu tunategemea kuwa na wanafunzi milioni moja ambao wanaenda kuanza kidato cha kwanza tunatarajia baada ya miaka minne tuwaone wanamaliza kidato cha nne, lakini kwa bahati mbaya wengine wanaweza wakadondoka hapo njiani alisema.

Alisema lengo ni kupunguza mdondoko kwa wanafunzi ili wote wanaoanza safar ya masomo waweze kumaliza salama.

“Kwa niaba ya serikali kama wasimamizi wakuu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Elimu kwenye mamlaka hizi, kwa niaba ya Wizara ya Elimu tunapenda kuwahakikishia KOICA, ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza mradi huu,”alisema.

Aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kutekeleza mradi huo kwa kuwa utakapofanya vizuri utapanua wigo kwa Halmashauri zingine kupata mradi huo.

“Kuna Mamlaka za Serikali za Mitaa 184, kama jitihada hizi zitafikia mamlaka zote tutaweza kukabiliana na mdondoko huu kwa kiwango kikubwa” alisema.

Alitoa wito kwa wazazi kuzuia mdondoko wa wanafunzi na kwamba afua zinazofanywa na serikali ni saidizi lakini wazazi ndio wanawajibu wa kuondoa hali hiyo.

“Hii itatusaidia sana kila mtoto anapata haki yake ya kupata elimu nchini, Rais ametuhakikishia kwamba matatizo ya elimu yanashughukiwa, ametoa fedha za ujenzi wa madarasa 15,000, tumuunge mkono Rais wetu kama ambavyo wadau wenzetu wa maendeleo wameliona hili na wanamuunga mkono,”alisema.

Naye, Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA, Kyucheol Eo, alisema miongoni mwa matatizo ya mdondoko ni wanafunzi kutembea umbali mrefu.

“Tanzania imefanya jitihada mbalimbali na kuongeza udahili wa wanafunzi, tutaendelea kuwa nanyi kwenye utekelezaji wa mradi wa EP4R, kuna mradi mwingine ambao januari 2022 baadhi ya Halmashauri zitanufaika na mradi huu,”alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa PWC, Nelson Msuya, alisema wao wamepokea fedha na kupeleka kwenye Halmashauri hizo ili mipango yao itekelezwe inavyotakiwa.

“Tunaomba sana fedha hizi zikafanye kazi iliyoombewa, tunaamini kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuweka kumbukumbu za utekelezaji wa mradi huu,miradi hii itafanyiwa ukaguzi tunaomba ilete matokeo chanja,”alisema.


Matangazo

  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert (extension) 1 May 28, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert (extension) May 28, 2025
  • TOR - Msimbazi Watershed Management – Modelling May 26, 2025
  • Monitoring & Support, TOR - DMDP 2 SWM Service Framework & Delivery System in Dar May 26, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Mhe. Katimba awapokea Wabunge wa Zambia waliokuja kujifunza kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara

    May 28, 2025
  • Mtwale Atoa Mwongozo kwa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa

    May 27, 2025
  • Nipo tayari kufanya kazi pamoja nanyi kufikia malengo ya Mhe. Rais – Prof. Tumaini Nagu

    May 26, 2025
  • TARURA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.