Swahili
  • English
  • Swahili
    • Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Machapisho
      • Taarifa za Mapato
      • Majarida
      • Fomu Mbali mbali
      • Presentations
      • Ramani za mradi wa BOOST
      • Program ya SCALE
    • Miongozo
      • Miongozo OR TAMISEMI
      • Miongozo ya Elimu
      • Green and Smart Cities
      • Miongozo ya Kilimo
      • Miongozo ya Afya
    • Michoro ya Ujenzi
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)
  • Maktaba ya Video

FMO’s Wakumbushwa Utendaji wao

Imewekwa tar.: March 29th, 2018
Dkt. Charles Mhina Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa wakati akifungua 
Semina ya Maafisa usimamizi wa fedha wa ngazi ya Mikoa (FMOs) katika Ukumbi wa 
OR TAMISEMI pembeni ni Mkurugenzi wa TEHAMA OR TAMISEMI Ndg. Erick Kitali.


Na Atley Kuni- OR TAMISEMI

Maafisa Usimamizi wa Fedha (Finance Management Officers – FMOs) kutoka Sekretarieti za Mikoa yote ya Tanzania Bara wamesisitizwa kuwa jicho la usimamizi wa fedha za Halmashauri na kutoa taarifa kwa Katibu Tawala (RAS) pamoja na ngazi ya Wizara ili kuwa na taarifa sahihi za kifedha kuanzia ngazi ya Halmashauri, Mkoa na Wizara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Charles E. Mhina wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ufuatiliaji wa Fedha zinazopelekwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (Fiscal Transfer Tracking Monitoring(FTTM) – Web Portal)  yanayowakutanisha FMOs kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara kuanzia tarehe 27-28 Machi, 2018 kwenye ukumbi wa Maabara ya Kompyuta uliopo katika jengo la Sokoine OR TAMISEMI, mjini Dodoma.

Dkt. Mhina amewahimiza Wataalam hao kuwa eneo la utoaji wa taarifa ni muhimu sana ili kuwa na taarifa sahihi zitakazosaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.

“Tulichobaini kama Wizara kuna umuhimu wa kuimarisha daraja la mawasiliano kati ya FMOs na Halmashauri. FMOs mmekuwa mkitoa taarifa kwa RAS na Wizara, huku mkisahau kwamba nyinyi kama wataalam mnatakiwa kuzisimamia na kuzijengea uwezo Halmashauri pia.” amesema Dkt. Mhina na kuongeza kuwa changamoto zilizopo zianishwe na kutumika kama chachu yakuleta mabadiliko.

“Changamoto ya matumizi sahihi ya mfumo wa FTTM – Web Portal kutokana na ukosefu wa mafunzo imekuwepo toka 2015. Sasa tumieni fursa hii ya mafunzo mtakayoyapata kikamilifu ilimtakapo ondoka hapa mlete mabadiliko chanya katika usimamizi wa fedha. Wataalam wetu wa TEHAMA na FEDHA kutoka OR TAMISEMI wapo tayari na wamejipanga kuwaelekeza kikamilifu.” alisema Dkt. Mhina.

Pamoja Wataalam hao kusisitizwa juu ya mfumo wa FTTM-Web Portal, Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA OR TAMISEMI, Ndg. Erick Kitali  hakusita pia kuwakumbusha Wataalam hao kuwa ifikapo Julai Mosi, 2018 Mamlaka zote za Serikali za Mitaa zitumie  toleo jipya la 10 la Mfumo wa Malipo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa  (Epicor 10) ili kwenda sambamba na mahitaji ya sasa.

Ndg. Kitali amewaambia wataalam hao kuwa OR TAMISEMI katika utendaji wake wa kazi hutegemea sana ushauri wa Wataalam kutoka ngazi za msingi ambapo ndipo walipo wananchi. Hivyo, aliwataka Wataalam hao kuzingatia mafunzo yatakayotolewa ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Erick Kitali Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA OR TAMISEMI, akisisitiza jambo kwa Maafisa 
usimamizi wa fedha wakati wa semina hiyo ya siku mbili mjini Dodoma.

 

Mmoja ya Maafisa wawezeshaji wa Semina hiyo kutoka OR TAMISEMI akitoa ufafanuzi wa 
awali kabla ya kuanza kwa semina hiyo ya siku mbili.

 

Shani Mangesho Afisa usimamizi wa fedha kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora akitoa ufafanuzi juu ya 
masuala mbali mbali kwenye mikoa wanayo yasimamia hususan ni masuala ya fedha.
Elisius Gujenji, Afisa fedha kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma 
akieleza kwa kifupi majukumu yao kama wataalam wa fedha kwenye Mikoa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA KATIKA SHULE ZA MSINGI KWA KADA YA ELIMU CHINI YA MRADI WA GPE - TSP May 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA MKATABA KWA KADA YA AFISA LISHE May 13, 2025
  • DMDP 2 Dar SWM Service Framework & Delivery System - REOI Advert May 12, 2025
  • Msimbazi Watershed Management - REOI Advert May 12, 2025
  • Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi April 02, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA - TAMISEMI 2025 March 15, 2025
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI

    May 23, 2025
  • PJT-MMMAM Yawezesha Uanzishwaji wa Vituo 206 vya Malezi ya Watoto Wadogo

    May 21, 2025
  • SERIKALI KUJENGA DARAJA LINALOUNGANISHA KIJIJI CHA NEGERO – KILINDI

    May 21, 2025
  • MHE. MCHENGERWA ABORESHA TAARIFA ZAKE KWENYE  DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    May 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Waziri Kairuki atoa maagizo DART
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Mfumo wa ugavi-Wizara ya Afya
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.