• Kituo cha Huduma kwa Wananchi |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
    • Taasisi za Wizara
    • Majukumu ya Idara na Vitengo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari Mpya
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Youtube Channel
    • Instagram
    • Twitter
    • Facebook
  • Machapisho
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
    • Green and Smart Cities
    • Miongozo ya Kilimo
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Michoro ya Ujenzi
    • Msimbazi Basin Development Project
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App
    • Nyaraka Mbalimbali
  • Mifumo
    • Mikopo ya 10% ya Halmashauri
    • Ajira za Elimu & Afya
    • Mfumo wa Tarifa za Shule (SIS)

Fedha za Uviko-19, zikatumike kwa malengo yaliyokusudiwa - Dkt. Dugange

Imewekwa tar.: September 17th, 2021

Na Atley Kuni-DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, anaye shughulikia Afya, Dkt. Festo Dugange, alihitimisha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, huku akiwaachia kazi kubwa yakwenda kufanya ikiwepo Matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya UVIKO-19 kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akifunga Mkutano huo wa mwaka wa Mwaka wa Waganga wakuu wa Mikoa Pamoja na Halmashauri jijini Dodoma tarehe 16, Septemba, 2021, Dkt. Dugange alisema, serikali imetoa fedha kwaajili ya Mpango Shirikishi na Harakishi wa Jamii dhidi ya Chanjo ya Uviko-19, hivyo viongozi wa Mikoa na Halmashauri wanajukumu lakusimamia kwa umakini ili fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Asitokee kiongozi yeyote kubadilisha matumizi ya fedha hizo” Alisisitiza Dkt. Dugange

Dkt. Dugange amewaambia Waganga wakuu hao kuwa Serikali inaendelea kupeleka fedha katika ujenzi wa vituo vya afya na katika hatua ya sasa, imepeleka bilioni 165.7 kwaajili ya ujenzi wa Hospitali 102, ukamilishaji wa maboma 555 na ujenzi wa vituo vya afya 71, ikiwa ni ukamilishaji wa bajeti ya 2020/21, na kuongeza kuwa kufikia Septemba 2021, jumla ya shilingi bilioni 37.5 zimepelekwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya afya kwenye tarafa 150 ambazo hazikuwa na vituo vya afya.

“Nichukue nafasi hii kuwaelekeza wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Pamoja na nyie wataalam, mkasimamie kwa ukamilifu ili majengo hayo yakamilike kwa wakati na yaendane na thamani ya fedha iliyo pelekwa” ameelekeza Naibu Waziri Dugange.

Katika hatua nyingine, Dkt. Dugange amewataka viongozi hao, wakasimamie vema majukumu yao ili wananchi waridhishwe na kuvutiwa kupata huduma   katika vituo vya afya vya serikali kila wanapo zihitaji, kwani itasadia kuongeza mapato na kujiendesha vyenyewe,  lakini pia kuondosha rufaa zisizokuwa za lazima, huku akihimiza matumizi ya Mifumo ya TEHAMA yatakayo saidia kuwa na taarifa sahihi za kitakwimu kwenye Vituo vyote.

Awali kabla Dkt. Dugange kufunga mkutano huo, Waganga Wakuu wa Mikoa Pamoja na Halmashauri, walitoka na maazimio tisa, ikiwepo kufunga mitambo ya kuzalisha hewatiba ya oksijeni katika kila Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Halmashauri, kutekeleza Mpango wa Jamii Shirikishi na Harakishi Dhidi ya UVIKO-19 ili kuongeza kasi ya watu kuchanjwa.

Maazimio mengine ni ilikuwa kuhakikisha Kamati za Usimamizi katika ngazi za Mkoa na Halmashauri, kusimamia miradi ya ujenzi iliyopo katika maeneo yao, aidha Wakurugenzi wa Halmashauri waweze kutenga fedha za tathmini na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Viongozi hao walikubaliana pia vituo vipya vilivyojengwa vianze kutoa huduma kulingana na majengo yaliyokamilika kwakutumia vifaa na rasilimali   watu iliyopo hasa utoaji wa huduma ya wagonjwa wa nje na ile ya Mama na Mtoto (OPD, RCH, nk.)

Aidha fedha za miradi ya maendeleo zitumike kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Miongozo na Taratibu ili zisivuke mwaka wa fedha, vilevile wadau waliopo kushirikishwa ndani ya Mikoa na Halmashauri ili kuchangia bajeti za Mikoa na Halmashauri kila mwaka kulingana na vipaumbele vilivyopo, sula lingine walilokubaliana ni kuandaa Mwongozo wa Uchangiaji gharama za huduma za Damu Salama.

Na mwisho walikubaliana kuwa na Miongozo wa Ukaguzi wa Bidhaa za Afya utakaotumika kwenye vituo vya huduma za afya ngazi ya mikoa na Halmashauri Pamoja na kuhuisha Mwongozo wa Mshitiri uliopo sasa.

Awali akiendesha kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa, anayeshughulia Afya, Dkt. Grace Magembe, aliuambia Mkutano huo kuwa, ili kufanikiwa katika Mpango Jamii, Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya Uviko-19, nimuhimu kuwatumia wataalamu waliopo ngazi za Mikoa na Halmashauri kwakuwa wao wapo karibu zaidi na jamii.

Mkutano wa huo wa Siku tatu, uliandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambapo ulifunguliwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima na kufungwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Festo Dugange, huku ukiwa umebebwa na kaulimbiu ya mkutano, “Ustahamilivu wa Mifumo ya Afya katika Mapambano dhidi ua UVIKO-19 ‘Changamoto na Fursa’’.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Serikalini kutoka Ofsii ya Rais -TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah, akiwa na Wanahabari 

wakongwe nchini kutoka Serikalini na kwenye asasi binafsi, akichangia  mada kuhusu umuhimu wakuwashirikisha 

maafisa habari wa Mikoa na Halmashsuri katika Mapambano dhidi ya Uviko-19


Ummya Wayayu, Mtaalam wa fedha kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, alipokuwa akifafanua masuala ya fedha katika kikao hicho

Dkt. Anna Nswila moja ya Madaktari wazoefu, ambaye amestaafu akitoa uzoefu kuhusu masuala 

mbali mbali ya Afya, ambapo alialikwa kwa ajili yakutoa uzoefu

Dkt. Grace Magembe, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI,akiwa anaongoza kikao cha Waganga Wakuu wa 

Mikoa na Halmashauri, uliomalizika mjini Dodoma


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA (Marudio) July 20, 2022
  • TANGAZO LA KAZI - TOA July 22, 2022
  • MAJINA YA WALIOPATA AJIRA KADA ZA AFYA NA UALIMU June 26, 2022
  • ORODHA YA WAKUU WA KITENGO CHA FEDHA YENYE MABADILIKO 5-5-2022 May 06, 2022
  • Kazi za muda za makarani na wasimamizi wa Sensa 2022 May 05, 2022
  • MUDA WA NYONGEZA MAOMBI YA AJIRA ZA TAMISEMI 2022 May 04, 2022
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • MJINI MAGHARIBI, PEMBA ZATWAA UBINGWA MPIRA WA MEZA

    August 17, 2022
  • ‘TAMISEMI NI MDAU MKUBWA WA TAKWIMU ZA SENSA’ BASHUNGWA

    August 17, 2022
  • Utekelezaji wa Miradi ya Elimu isimamiwe na kukamilika kwa wakati- Dkt. Msonde

    August 15, 2022
  • UBUNIFU KIVUTIO UMISSETA 2022

    August 15, 2022
  • Angalia zote

Video

Taarifa ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri, kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/22
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Michoro ya Ujenzi
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Ajira za Tamisemi
  • Mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania

    Simu: +255 262 321 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.